KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 24, 2011

Inter kukutana na Manchester City kujadili mpango wa mkopo wa Carlos Tevez Inter Milan imeonyesha nia ya kumtaka Carlos Tevez kwa mpango wa mkopo wa muda mrefu ndani ya msimu huku mpango mzima wa kumchukua kwa minajili ya uhamisho wa moja kwa moja ukisubiri mpaka majira yajato ya kiangazi
Klabu hiyo imejipanga kukutana na viongozi wa Manchester City July 31 kujadili uwezekano huo “Corriere dello Sport”.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Boca Juniors ameshatanabaisha kutaka kuondoka Eastlands huku akitazamiwa kutaka kurejea nchini Brazil katika klabu ya Corinthians kabla ya mpango huo kuvunjika
Licha ya kwamba ya mpango wa uhamisho kuelekea Corinthians kuonekana kukwama kutokana ada kubwa ya uhamisho kutakiwa na mwajiri wake wa sasa kikosi cha Gian Piero Gasperini kinaonekana kutoa suluhu ya hilo.

Kama ilivyokuwa kwa Zlatan Ibrahimovic alipotoka Barcelona kuelekea AC Milan ilivyokuwa uwezekano wa namna hiyo unaweza kufanyika na kukubaliwa kabla ya wakati wa uhamisho wa mkopo kuanza .
Wazee wa Giuseppe Meazza walianzisha mpango wa kubadilishana mchezaji akihusishwa Mcameroon Samuel Eto'o mpango ambao n I maarufu kama “swap deal”lakini badala yake ilionekana kama walikuwa tayari kulipa euro milioni €45 ambazo zilikuwa zinatakiwa na Roberto Mancini.


No comments:

Post a Comment