KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 24, 2011

Fifa yampiga yamfungia Mohamed Bin Hammam maisha baada ya kujihusisha na rushwa katika soka Shirikisho la kandanda duniani Fifa imemfungia maisha Rais wa zamani wa AFC ambaye pia ni mjumbe wa shirikisho hilo Mohamed Bin Hammam kutojihusisha na vitendo vyovyote vinafanana na kandanda baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na mambo ya rushwa kufuatia kikao cha siku mbili kilichokuwa kinasikiliza tuhuma juu yake za rushwa ndani shirikisho hilo.
Hammam mwenye umri wa miaka 62 walisimamishwa na fifa tangu May 29 sambamba na mjumbe mwingine wa kamati ya utendaji Jack Warner baada ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa tuhuma ambazo zilitolewa na muungano wa soka la Caribbean “Caribbean Football Union” ya kwamba walitoa rushwa katika kampeni za kuwania Urais wa fifa .

Kadhalika, baada ya kikao cha siku mbili cha kusikiliza kesi hiyo ,mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Petrus Damaseb ametangaza kuwa Bin Hammam amekutwa na makosa hayo na amefungiwa kujihusisha na shughuli zozote zinazo husiana na soka katika maisha yake yote.
Anakaririwa Damaseb akisema
"Bin Hammam is hereby banned from taking part in any kind of football-related activity at national and international level for life,"


No comments:

Post a Comment