KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 24, 2011

Drogba ana matumaini na kuongezwa mkataba Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba ambaye kwasasa ana umri wa miaka 33 ana matarajio makubwa ya kuongeza mkataba wake mwingine na klabu yake mkataba ambao utaendelea kumuweka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika kitongoji cha Stamford Bridge mpaka 2013.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya The Ivory Coast ambaye alijiunga na Blues akitokea Marseille mwaka 2004 ametanabaisha kuwa mazungumza yalikwisha kuanza juu ya kuongeza kwake mkataba.
Anakaririwa akisema
"tumeanza mazungumzo,kila mtu anajua jinsi ninavyo ipenda Chelsea na ndicho ninacho kitaka.
"sina shaka nitaendelea kuwepo hapa mpaka msimu ujao .nilisema mwaka uliopita kuwa nitaendelea kusalia hapa mpaka kumalizika kwa mkataba wangu nab ado nipo"
"sasa nataka kuendelea licheza soka hapa na kujitolea kwa moyo wangu wote kama ambavyo nimekuwa nikifanya.
"huu utakuwa ni msimu wangu wa nane ndani ya klabu hii na hiyo ina maana kubwa kwa kila mshambuliaji kusalia ndan I ya Chelsea kwa muda mrefu."
Kwa mara ya kwanza mshambuliaji huyo ndani ya soka lake katika klabu hiyo ameshindwa kujinasibu juu ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza ndani ya msimu huu.
Mshambuliaji huyo mwenye misuli anajipanga kufikia rekodi ya Fernando Torres ya kuwepo katika kikosi cha kwanza chini ya bosi mpya Andre Villas-Boas ambaye ameanza kutamani kuongeza mshambuliaji mwingine.

No comments:

Post a Comment