KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 24, 2011

Kaka: Jose Mourinho anataka nisalie Real Madrid Kiungo mchezeshaji wa Real Madrid Ricardo Kaka amesisitiza kuwa hataondoka katika jklabu yake hiyo kwa kuwa kocha wake Jose Mourinho amemshauri atakuwa katika furaha endapo ataendelea kusalia katika klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akihusishwa na kutaka kuondoka kutoka katika jiji kuu la Hispania kufuatia kuendelea kusumbuliwa na maumivu ambayo amekuwa akihangaika nayo tangu alipohamia katika klabu hiyo mwaka 2009 akitokea AC Milan.
Kaka alikuwa akiripotiwa kutakiwa na vilabu viwili ikiwa ni pamoja na klabu yake ya zamani ya AC Milan na wapinzani wao wakubwa Inter Milan lakini sasa anaweka wazi kuwa hakuna haja ya kuondoka katika klabu hiyo.
Akikaririwa na gazeti la Marca Kaka anasema
"siku zote nilikuwa nitaka kusalia na ninataka kuicheza Real Madrid n a kutoa ushauri"
"marafiki zangu mara zote wamekuwa wakinisaidia,kitengo cha ufundi .nimekuwa nikifahamu kutakuwa na tetezi nyingi lakini nimezungumza na klabu na kocha amelimaliza
" I do not want to leave and the coach told me he wants me here for next season and the club told me there is no need to sell me."


No comments:

Post a Comment