KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 24, 2011



Kocha mzoefu Carlos Alberto Parreira anaamini kuwa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kipo katika kipindi cha mpito na wachezaji kama Alexandre Pato wa AC Milan na Neymar na Ganso wa Santos wanapaswa kuwa ngangari kama timu hiyo ya taifa ya Brazil itataka kuwa katika mafanikio zaidi.
Brazil ilishindwa kung’ara katika Copa America kufuatia kutolewa na Paraguay katika hatua ya robo fainali na Parreira aliingoza Brazil kwa mafanikio katika fainali ya kombe la dunia 1994 akidhani kuwa timu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa katika siku za usoni
Akikaririwa katika mkutano na waandishi wa habari Perreira anasema
"kwasasa tuna timu mpya ya Brazil na yenye vijana wazuri kama Pato, Neymar na Ganso. Timu ambayo inafanana na ile ya akina Cafu, Ronaldo, Rivaldo, Ronaldinho na Kaka kwa hiyo changamoto ni kubwa .vijana hawa bado wana mengi ya kujifunza na wanapaswa kuonyesha ukomavu kidogo".
"timu inatakiwa kuwa imara katika idara zote mbele na nyuma.uzuri wa mchezo ni timu kuwa na mizani sawa sehemu zote. Brazil ilishinda kombe la dunia mwaka 1970 baada ya kufunga magoli 19 na kufungwa saba."
Brazil haihitaju kufuzu katika mchekato wa kuelekea katika kombe la dunia mwaka 2014 kufuatia kufuzi moja kwa moja kwa kuwa watakuwa ni wenyeji wa fainali hiyo.

No comments:

Post a Comment