Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney anasema Liverpool itabadilika katika msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda nchini Uingereza .
Liverpool ambayo ilimaliza katika nafasi ya sita katika msimu wa ligi uliomalizika imewasajili kiungo Jordan Henderson, Charlie Adam na Stewart Downing katika kipindi cha usajili wa cha majira ya kiangazi.
Anakaririwa akisema
"Liverpool imefanya usajili wachezaji wazuri,".
"ninaamini watapigana kwa nguvu zote nadhani watakuwa na fikra za kushinda taji."
Mchezaji huyo wa zamani wa Everton ameendelea kwa kusema
"nafasi kubwa au ushindani mkubwa utakuwa ni kwa Chelsea, Liverpool, Arsenal na Manchester City.
"timu moja kati ya hizi ukijumla na sisi watakuwa katika vita ya kutwaa taji."
Rooney atakuwa katika dhamira ya kutwaa taji la tano la ligi kuu ya uingereza akiwa na United,lakini angependelea kuona akianza msimu kwa kuwachapa mabingwa wa FA Cup Manchester City katika mchezo wa ufunguzi wa msimu katika ile “Community Shield” mchezo ambao utapigwa katika dimba la Wembley August 7.

No comments:
Post a Comment