Ryan Giggs anaamini kuwa uzoefu mkubwa wa Manchester United unaweza kuwa ni kigezo cha kuamua kuukimbiza ubingwa wa Premier League msimu huu.
United inafanana kipoints na Manchester City na wanashindwa na wapinzani wao idadi ya magoli.
Hata hivyo Blues kwa maana ya City wanaonekana kucheza michezo mingi na vigogo ama timu sita za juu ikiwa ugenini ikilinganishwa na Red Devils Man united ambayo imecheza michezo mingi Old Trafford,ukiachana na mchezo dhidi ya Liverpool, na ule wa dhahama ya mabao 6-1 toka kwa Man City mwezi October.
Bado Giggs anadhani nafasi yao ya kutengeneza rekodi nyingine ya kutwaa taji hilo kwa mara ya 13 mwezi May itategemea ni timu gani akili inafanya kazi zaidi katika mbio hizi lakini anadhani United ipo katika jaribio hilo.
No comments:
Post a Comment