CHAMPIONS
LEAGUE
Venue: Estadio da luz
Bosi wa Benfica
Jorge Jesus ametamba kujibu tambo za mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba kwa
kuwachapa Chelsea mjini katika mchezo wa ligi ya mabingwa usiku huu mjini Lisbon.
Jesus amekubaliana
na mshambuliaji huyo lakini akisema pengine alikuwa akitania na kusema
anachojua ni kile anachofikiri.
Ananukuliwa akisema
"kwa
kile kitakachotokea itakuwa ni kujibu aliyosema na kitaelekea kwa Drogba na
kudhihirisha kuwa sisi ni bora kuliko yeye"
Alichokisema
Drogba kupitia video ni kwamba wanachokitazama ni kwenye nusu fainali ngumu
dhidi ya mabingwa watetezi Barcelona na kusahau msemo wa Kiswahili kuwa
usitukane mamba kabwa hujavuka mto.
Sasa Jorge jesus
anajibu kauli ya mshambuliaji huyo
Hii maana
yake Drogba anaitazama Barcelona kwa kuwa Barcelona are a very, very big team.
Amesahau kuwa
timu yake ya Chelsea inajua kuwa Benfica ilivyopanda milima na kuvuka mabonde
kufikia hatua hiyo
Chelsea in the Champions League
•2010-11: Lost 3-1 to Manchester
United in QF
•2009-10: Lost 3-1 to Inter Milan in
last 16
•2008-09: Lost on away goals to
Barcelona in SF
•2007-08: Lost on penalties to
Manchester United in final
•2006-07: Lost on penalties to
Liverpool in SF
Bosi wa Chelsea
Roberto di Matteo imejitete kuwa wanakiwango cha ubora cha kutosha licha ya
kuwa katika hali mbaya kimatokeo msimu huu.
Kiungo wa Chelsea
Frank Lampard anasema wachezaji hawakuwa vizuri kama ilivyotokea wiki iliyopita.
Branislav
Ivanovic amesafiri kuelekea Lisbon licha ya kukosekana katika mchezo wa sare ya
bila magoli katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham kufuatia kuwa na
maumivu.
Kiungo wa
kati wa Benfica Luisao anatarajiwa kuwapo kikosini na akitarajiwa kutengeneza “partnership”
na Jardel wakati ambapo mlinzi Ezequiel
Garay akiwa katika hatihati ya kuwepo katika mchezo wa leo.
Mfungaji mahiri
(Top-scorer) Oscar Cardozo na Rodrigo wanatarajiwa kuongoza sehemu ya
ushambuliaji kwa wenyeji usiku huu.
Apoel Nicosia v Real Madrid
Kiungo wa Apoel
Nicosia raia wa Brazilian Gustavo Manduca anatarajiwa kutokuwepo dimbani
hii leo katika mchezo wa ligi ya mabingwa
dhidi ya vinara wa ligi kuu ya nchini Hispania Real Madrid baada ya kuondoshwa
katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.
Badala yake
kocha Ivan Jovanovic atafanya uchaguzi mwingine .
Madrid itakuwa
dimbani bila ya Lassana Diarra, Angel di Maria, Jose Callejon na Ricardo
Carvalho wote wakiwa ni majeruhi.
Kiungo Xabi
Alonso amesimama kwa adhabu lakini Mesut Ozil kiungo mchezeshaji anarejea baada
ya kibano cha kutumikia adhabu ya mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Real
Sociedad.
Jovanovic anasema
changamoto iliyopo ni kwa mabingwa hao mara tisa Madrid hii katika robi fainali
kuonyesha uwezo wao mpaka mwisho.
Mpaka kufikia
hapo Apoel ilikuwa katika kundi
lililokuwa na timu kama FC Porto, Shakhtar Donetsk na Zenit St Petersburg na katika hatua ya 16 bora
iliindosha timu ya Lyon.
Ananukuliwa Jovanovic
akisema
"sisi
ni timu ndogo ulaya lakini tuna moyo mkubwa " .
Bosi wa Bolton
Owen Coyle amesema hajua ni jinsi gani vijana wake watafanya kuelekea katika
mchezo wa hii leo marudiano wa michuano ya FA katika dimba la White Hart Lane.
Kikosi cha Coyle
kitakuwa na kazi kubwa ya kukutana dhidi ya Tottenham mchezo uliopangwa upya
baada ya kuvunjika kufuatia Fabrice
Muamba kuzimia ghafla uwanjani March 17.
Ananukuliwa akisema
"tutafanya
kile kinacho takiwa kwa kadri ya uwezo wetu kama tunavyofanya mara zote .
Kauli yake
pia inakuja wakati huu ambapo hali ya afya ya Muamba ikiimarika.
Anaendelea kunukuliwa
akisema
"lakini
siwezi kusema itakuwaje mpaka tutakapo kuwa pale uwanjani."
Muamba anaendelea
kuimarika kiafya huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa akiweza kutoka
kitandani na kuanza kula.
“Because Fabrice anaendelea vizuri nah ii inaturuhusu
sisi kucheza mchezo huu”
Inter Milan imemfukuza kazi Claudio
Ranieri baada ya matokeo mabaya
Inter Milan imemfukuza
kazi kocha wake Claudio Ranieri baada ya kuwa na matokeo mabaya katika ligi
akiwa ameshinda mchezo mmoja katika michezo kumi iliyopita ya ligi kuu ya
nchini Italia maarufu kama Serie A.
Bosi huyo wa
zamani wa Chelsea alianza kazi San Siro mwezi September akichukua nafasi ya Gian
Piero Gasperini baada ya kuwa kazini kama incherge wa benchi la ufundi kwa
michezo mitano tu.
Wataalamu wa
mambo ya soka nchini Italia wanasema
"inashangaza
kwa kuwa kila mtu alijua kuwa angeendelea mpaka kumalizika kwa msimu . Alionekana
kama ni mtu ambaye pengine angewabana wachezaji wakongwe lakini inaonekana
msimu unazidi kusonga mbele na wachezaji hao wakongwe wanaendelea kupata nafuu
ya uwepo wake.
Laurent
Blanc na Andre Villas-Boas wanatazamwa kumrithi nafasi yake.
Jana Rais wa
klabu Massimo Moratti alinukuliwa akisema "I think that Claudio Ranieri will remain
until the end of the season."lakini sasa mambo yenda tofauti
Kwasasa kocha
wa vijana Andrea Stramaccioni anakuwa katika benchi la Inter maarufu kama Nerazzurri.
Stramaccioni
anasifa ya kuongoza kikosi cha vijana wadogo wa Inter ambao walitwaa taji la NextGen mbele ya
vijana wa Ajax jumapili iliyopita.
Baada ya
kipigo cha jumapili toka kwa Juventus, Inter imekalia nafasi ya nane katika Serie A, points 22 nyuma ya wapinzani wao
wakubwa ambao wanaongoza ligi hiyo.
Mapema mwezi
huu waliondoshwa katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa na Marseille
earlier this month.
Manchester United juu!
Mshambulizi Wayne
Rooney alihakikisha timu yake Manchester United inapanda kileleni mwa ligi kuu
ya Uingereza kwa kuichapa Fulham bao moja bila.
Bao hilo
lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea
pasi safi kutoka kwa Jonny Evans.
Kwa ushindi
huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu.
Kufikia sasa
timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.
Manchester
City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya
jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland.
Vijana hao
wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya
Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn.
Hata hivyo
mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti.
Hii ni baada
da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha mshambulizi
Danny Murphy katika eneo la hatari katika dakika ya 87.
meneja huyo
wa Fulham amenukulikwa akisema kuwa kila mtu aliyeshuhudia mechi hiyo
alitarajia wapewe penalti.
Ahly "haikufurahia" adhabu
ya al-Masry
Klabu ya Al
Ahly ya Misri imesema "wameshangazwa na kuhuzunishwa" na uamuzi wa
kuifungia klabu ya al-Masry kucheza ligi kwa miaka miwili.
Vigogo hao
wa kandanda wa Cairo wanaamini adhabu hiyo iliyotolewa na Chama cha Kandanda
cha Misri siku ya Ijumaa ingekuwa kubwa zaidi ya hiyo.
Mashabiki 74
walikufa mjini Port Said wakati al-Masry ilipoikaribisha Al Ahly tarehe 1 mwezi
wa Februari.
"Tumehuzunishwa
na kwa kweli tumekasirishwa," mjumbe wa bodi ya Al Ahly Khaled Mortagy
aliiambia BBC.
"Tunaamini
haki haikutendeka, inapotokea mashabiki 74 wamekufa katika uwanja wa nyumbani
wa klabu hii na bado hii ndio adhabu wanayopewa, ni mwaka mmoja tu wanafungiwa
kucheza."
"Kwa
sababu, kinadharia, msimu huu umemalizika, kwa hiyo wanaposema wanafungiwa
miaka miwili, maana yake halisi ni mwaka mmoja tu."
Wakati msimu
wa sasa wa ligi ya Misri ukiwa umefutwa tangu kulipotea ghasia za Port Said,
al-Masry wataanza kucheza tena soka kwa msimu wa 2013/2014 - ikiwa na maana
watakosa msimu wa mwakani tu.
Klabu hiyo
ya Port Said pia imefungiwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani kwa muda wa miaka
mitatu.
Baada ya
al-Masry kushinda mabao 3-1 tarehe 1 mwezi wa Februari, mashabiki wake walivamia
uwanja na kuwashambulia wachezaji na mashabiki wa Al Ahly.
Wiki
iliyopita Mwendesha Mashtaka mkuu wa Misri aliwafungulia mashtaka ya mauaji na
uzembe uliosababisha ghasia watu 75.
Mortagy
alisema angependa kuona al-Masry ikifungiwa kushiriki Ligi Kuu kwa angalao muda
wa miaka mitano, akitolea mfano unaopaswa kufuatwa ilipofungiwa klabu ya
Liverpool baada ya mkasa wa Heysel wa mwaka 1985.
Katika tukio
hilo, klabu hiyo ya England ilifungiwa kushiriki mashindano ya Ulaya kwa muda
wa miaka sita baada ya mashabiki wake kuonesha utovu wa nidhamu uliosababisha
vifo vya mashabiki 39, wengi wakiwa wa klabu ya Juventus.
Licha ya Al
Ahly kukusudia kukata rufaa kutokana na uamuzi wa Chama cha Kandanda cha Misri,
bodi ya klabu hiyo tayari imeshaamua kutocheza mechi yoyote mjini Port Said kwa
muda wa miaka mitano ijayo.
Mabingwa hao
mara sita wa Afrika, hawakufurahishwa pia na uamuzi wa kuwataka wacheze mechi
zao nne katika uwanja usio na watazamaji, baada ya baadhi ya mashabiki wake
kufyatua na kurusha miale ya moto, wakati kocha wao Manuel Jose na nahodha
Hossam Ghaly pia wamefungiwa mechi nne kwa kuzozana na maafisa.
Andy Roddick amchapa Roger Federer katika
Miami Masters
Roger
Federer ambaye anarekodi ya kushinda michezo 16 ya michezo ya Miami Masters
amefikia mwisho baada ya kuchapwa 7-6
(7-4) 1-6 6-4 na Andy Roddick katika mzunguko wa tatu wa michezo ya Miami
Masters.
Baaba ya
kichapo hicho amenukuliwa akisema jamaa huyo raia wa uswiz akisema
"nimetota
leo “I came out flat today” ,"
“I was a bit
tired, I guess."
Nyota namba
moja katika mchezo wa tennis Novak Djokovic yeye amefanikiwa kupata nafasi
katika round ya nne baada ya ushindi wa 6-3 6-4 dhidi ya mwenzake msebia toka
taifa moja Victor Troicki.
Upande wa
wanawake nyota namba moja duniani katika
mchezo huo Victoria Azarenka amesonga mbele kuelekea robo fainali baada ya
kumchapa mwanadada toka Slovakia Dominika Cibulkova 1-6 7-6 (9-7) 7-5.
Wladimir Klitschko anajipanga kutete
taji
Bingwa wa
uzito wa juu katika masumbwi Wladimir Klitschko anatarajiwa kutete taji lake la
12 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Tony Thompson mchezo ambao umepangwa
kufanyika July 7 baada ya mpango huo
kuwekwa mezani jana na huku mshauri wa , Klitschko Shelly Finkel akiongea na
vyombo vya habari.
Hili litakuwa
ni pambano la kama kulipiza kisasi.
No comments:
Post a Comment