Mabao mawili
yaliyofungwa na Papiss Cisse yamezidi kuiongezea Newcastle hamu ya kucheza
mashindano ya Ulaya msimu ujao baada ya kuongeza machungu kwa Liverpool
iliyocheza na wachezaji 10 tu katika pambano la Ligi Kuu ya Kandanda ya
England.
Cisse
alitumbukiza mpira kwa kichwa baada ya kulishwa mpira wa juu na Hatem Ben Arfa
katika kipindi cha kwanza kabla ya kufunga bao la pili alipopokea pasi ya Demba
Ba katika nusu ya pili ya mchezo.
Kiwango cha
chini ya kandanda kilichooneshwa na Liverpool, ambapo mshambuliaji wao wa kati
Andy Carroll alioneshwa kadi ya manjano baada ya kujiangusha kwa makusudi
katika eneo la Newcastle, pia ilishuhudia mlinda mlango wao Pepe Reina kutolewa
nje kwa kuoneshwa kadi ya nyekundu.
Na kwa sasa
Liverpool wamekwishapoteza michezo sita kati ya saba ya ligi.
Reina
alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuchezewa rafu na James Perch alipokuwa
akijiandaa kufunga mpira uliopigwa na Mike Williamson.
Lakini baada
ya kugongana na mlinzi huyo wa Newcastle, Reina alimtwanga kichwa Perch na
mwamuzi Martin Atkinson hakuwa na njia nyingine ya kufanya ila kumtoa nje kwa
kadi nyekundu.
Kilikuwa
kipindi kingine cha kushuhudia vijana wa Kenny Dalglish wakinyanyaswa, ambao
katika msimamo wa ligi wanashikilia nafasi ya nane, pointi 11 nyuma ya Chelsea
wanaoshikilia nafasi ya tano.
Na kwa
wenyeji Newcastle, matokeo hayo yamewainua na kufikisha pointi sawa na Chelsea
wakiwa wanatafuta nafasi muhimu ya kumaliza msimu kwa kucheza Ligi ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment