Meneja wa
Manchester City Roberto Mancini, ameonesha matumaini mahasimu wao Manchester
United watapoteza pointi katika mbio zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya
England msimu huu.
Baada ya
Manchester City kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Sunderland, Manchester United
iwapo itailaza Blackburn siku ya Jumatatu itaiacha nyuma City kwa pointi tano.
"Nadhani
Jumatatu Manchester United huenda nao watatoa sare," alisema Mancini.
"Katika michezo minane inawezekana kutoka sare miwili. United inaweza
kukabiliwa na wakati mgumu.
Matokeo
dhidi ya Sunderland yameibakiza Manchester City nafasi ya pili ikiwa na pointi
71 na michezo saba kibindoni, wakati Manchester United inaongoza kwa
kujikusanyia pointi 73 na imebakisha michezo minane.
Lakini Man
United imeweza kushinda michezo miwili tu kati ya safari zake nane za michezo
ya ligi kwenye uwanja wa Ewood Park na Mancini ametabiri watateleza kwa mara
nyingine.
Mancini
ameelezea mechi dhidi ya Sunderland ilikuwa "pambano gumu, lililojaa
msisimko " baada ya Man City kuwa nyuma kwa mabao 3-1 na walipigana kiume
na kujipatia angalao pointi moja.
"Nadhani
yalikuwa matokeo sahihi, kutoka sare, lakini hatukucheza vizuri," Mancini
alilalama.
"Nilifurahia
dakika 10 za mwisho, kwa dakika nyingine 80 sikuwa na furaha kwa sababu
hatukucheza vizuri sana. Sijui kwa nini.
Akizungumzia
safari yao ya siku ya Jumapili ijayo kuikabili Arsenal katika uwanja wa
Emirates, Mancini amesema: "Nina hakika tutafanya vizuri kuliko mechi ya
Sunderland.
Meneja wa
Sunderland Martin O'Neill amesema kuna nafasi nyingi katika mbio za kuwania
ubingwa.
"City
ina kikosi chenye ubora wa hali ya juu," alisema.
"Kutakuwa
na heka heka za hapa na pale kabla msimu haujamalizika na Manchester United
watakabiliana nasi kwetu katika mechi ya mwisho kumalizia msimu."
No comments:
Post a Comment