Bayer yamfukuza kocha Dutt
Bayer
Leverkusen imemfukuza kazi kocha wake Robin Dutt baada ya kichapo cha mabao 2-0
toka kwa Freiburg.
Klabu hiyo
imetangaza hilo asubuhi ya leo na nafasi yake kushikiliwa na kocha Sami Hyypia,
mlinzi wa zamani wa Liverpool na bosi wa
kikosi cha wachezaji vijana Sascha Lewandowski na watakalia nafasi hiyo kwa
mujibu wa taarifa ya klabu hiyo mpaka kumalizika kwa msimu.
Kichapo toka
kwa Freiburg ni channe ikiwemo kichapo cha michuano ya ligi ya mabingwa toka
kwa Bercelona cha mabao 7-1 on aggregate..
Wasaidizi wa
Dutt Damir Buric na Marco Langner pia wameondoka klabuni hapo.
Bao la Robben laipa nguvu Bayern
Bao la Arjen
Robben la dakika ya 69 lilitosha kuipa ushindi Beyern Munich dhidi ya Nurnberg
katika mchezo ambao ulionekana kama kama Bavarian derby matokeo ambao
yameisogeza Bayern Munich mbele zaidi kwa points tatu mbele ya Borussia
Dortmund katika kilele cha ligi kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Mdutch huyo
alifunga bao hilo katikati ya kipindi cha pili na kukipa kikosi cha kocha Jupp
Heynckes ushindi waliokuwa wakiusaka na hivyo kuipa jakamoyo Dortmund wao wakiwa
kileleni.
Hicho ni
kipigo cha nne mfululizo kwa Nurnberg na kimewashusha kwa points tatu katika
mstari wa hatari ya kushuka daraja na wakiwa wamesaliwa na michezo sita kabla
ya kumalizika kwa msimu
Bayern inatarajia
kukutna uso kwa uso na mabingwa mara sita wa taji la soka la nchini ujerumani Dortmund
jumamosi ijayo.
Henry apiga hat-trick
Thierry
Henry aliyerejea nchini marekani katika klabu yake ya New York Red Bulls
ameendeleza makeke yake baaya ya kufunga mabao matatu ndani ya mchezo mmoja yaa
“hat-trick” katika mchezo wa ushindi wa timu yake wa mabao 5-2 dhidi ya Montreal
Impact katika ligi ya nchi hiyo MLS.
Nyota huyo
wa zamani na mwenye heshima kubwa katika klabu ya washika bunduki wa Uingereza Arsenal
alifunga bao lake la kwanza kunako dakika ya 28 akinyamazisha furaha ya
wapinzani wao waliotangulia kwa bao la Sanna Nyassi lakini Justin Mapp akarejesha
tena baadaye furaha ya Montreal kwa bao la pili la dakika ya 38 ya mchezo.
Kenny Cooper
akafunga bao la penatina la kusawazisha
na kupelekea sare ya mabao 2-2 mpaka mapumziko kabla ya Red Bulls kuanza karamu katika
kipindi cha pili.
Henry alifunga
bao lingine dakika ya 56 huku naye Mehdi Ballouchy akiongeza la nne kunako
dakika ya 72 ikiwa ni dakika tatu tu baada ya kuingia akitoke benchi.
Henry alimalizia
hat-trick dakika moja kabla ya mchezo kumalizika.
Katika
mchezo mwingine Real Salt Lake ilipata mabao mawili katika dakika mbili za
mwisho za mchezo na kuipa ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Portland Timbers ushindi
ambao umewaweka katika kilele cha msimamo wa ligi ya Western Conference.
Alvaro
Saborio aliwapeleka wageni kwenye uongozi kunako dakika ya 38 kwa bao la mkwaju
wa penati lakini Darlington Nagbe
aliweka mambo sawa baada ya mapumziko kwa Portland.
South
Africa U-20 side beaten at home by Ghana
Timu ya taifa ya wanawake ya nchini
Afrika kusini ya wachezaji wenye umri chini ya miaka U-20 maarufu kama Basetsana na si “banyana banyana”
ambayo ni ya wakubwa imekubali kichapo
cha mabao 2-0 nyumbani toka kwa timu ya taifa ya Ghana ya wenye wenye umri huo
ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa michuano ya kusaka tiketi ya kufuzu
fainali ya michuano hiyo dunia fifa 2012
Kichapo hicho cha wenyeji kimekuja
wakiwa nyumbani katika mchezo uliopigwa Sinaba Stadium huko Daveyton.
Basetsana ilikuwa katika hali mbaya
katika kipindi cha pili baada ya kupigwa mabao mawili toka kwa wafungaji Florence
Dadson na Elizabeth Addo kiasi akina dada wa Ghana maarufu kama “Black
Princesses” kuwa mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili
zijazo.
Timu zote mbili katika cha kwanza
zilikuwa katika kiwango safi na vinavyo fanana kabla ya Dadson katika kipindi
cha pili kufunga bao la uongozi ikiwa ni dakika ya 50
Juhudi za Basetsana kusawazisha
hazikuzaa matunda na zilzidi kupotea baada ya Patience Hlongwane kusababisha penalt
akifanya madhambi katika eneo la hatari na yeye mwenyewe kutolewa nje kwa kadi
nyekundu penati hiyo ilifungwa na Addo na kuwa bao la pili kwa ghana.
Kombe la dunia la FIFA la wachezaji wenye umri wa chini ya miaka U-
20 Women's World Cup 2012 litachezwa nchini Japan baadaye mwaka huu
No comments:
Post a Comment