KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, April 1, 2012

Kenya Premier League : Sofapaka yachapwa


Timu ya AFC Leopards ya Kenya imeendelea kukalia usukani wa ligi kuu ya nchini humo “Kenya Premier League (KPL)” wakiwa na points 20 kufuatia matokeo mabaya ya wapinzani wao wakubwa katika kulikimbilia taji Sofapaka kupoteza mchezo wao mbele ya Chemelil Sugar katika mchezo mzuri wa mfululizo wa michezo ya ligi hiyo.
Bao lililowaangusha Sofapaka lilifungwa katika dakika ya 53 na Wycliffe Opondo kwa shuti kali ambalo lilimgonga mlinzi wa Sofapaka Duncan Ochieng.
Michezo mingine  Thika United imeendeleza wimbi lake la ushindi ambapo hapo jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Karuturi Sports mchezo uliopigwa katika mji wa Naivasha.
Bao hilo la ushindi liliwafanya wenyeji kunyamaza kimya kama wamemwagiwa maji na likifungwa na mfungaji anayeongoza katika kupachika mabao kwa sasa katika ligi hiyo maarufu kama KPL epha Aswani kunako dakika ya 75 ya mchezo.
 Mpaka sasa ana mabao 7 katika jumla ya michezo 7.
    Kule Bukhungu Stadium maeneo ya Kakamega, Western Stima imerejea katika mfululizo wa ushindi licha ya kupoteza wiki iliyopita kwa AFC AFC leopards katika uwanja huo huo.
  Baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 juma lililopita wageni safari hii wameibuka na ushindi kama huo dhidi ya Sony Sugar. Mabao hayo yamewekwa kimiani na  Alloys Mangi na Steve Biko kunako dakika za 20 na 60 ilhali bao la kufutia machozi kwa Sony likifungwa na Isaiah ‘Song”Omondi.
 

No comments:

Post a Comment