Thika United stun Sofapaka in the
Kenya Premier league
Mpira wa
adhabu ndogo wa moja kwa moja uliopigwa na Dennis Odhiambo ulitosha kuipa
ushindi Thika United wa bao 1-0 dhidi ya Sofapaka fc katika ligi ya kandanda ya
nchini Kenya premier league (KPL) mchezo ulipigwa Nyayo national stadium jiji Nairobi
hapo jana sunday.
Odhiambo alifunga goli hilo pekee katika dakika ya 45
kufuatia kiungo wa Sofapaka Anthony
Kimani kumfanyia madhambi Clifton Miheso
umbali wa yard 35 kutoka langoni mwa Sofapaka.
Nairobi City Stars……………………...0
Chemelil Sugar………………..0
Van Persie nets PFA award
Mshambuliaji
wa Arsenal Robin van Persie ametajwa kuwa Professional Footballers' Association
wa mwaka.
Van Persie
mwenye umri wa miaka 28 amefunga jumla ya mabao 27 katika ligi kuu ya Uingereza
Premier League msimu huu akiwa na timu yake ya washika bunduki na ni kutokana
na matunda kampeni yake kubwa katika klabu yake na kwa heshima kubwa
kutambuliwa na kupewa tuzo hiyo.
Ananukuliwa
mwenyewe Van Persie akisema
''kama watu
wengine wanasema it is special,lakini ni zaidi ya special ''
Hii ni
kwasababu unacheza dhidi yao wiki baada ya wiki na kila mmoja anafanya kila
liwezekenalo kushinda na mwishowe wanaweka mawazo yao kuwa mimi ni mimi ndiye “best
player” ni heshima kubwa ''
Tuzo ya
mchezaji kinda wa mwaka imekwenda kwa mlinzi wa pembeni wa Tottenham Kyle
Walker.
Nyota huyo
mwenye umri wa miaka 21 wa Spurs amewashinda wenzake kama akina Sergio Aguero na
Danny Welbeck na kushinda tuzo ambayo
imekuja kama kama “surprise” kwa mchezaji huyo wa zamani wa Sheffield.
Wote pia
wamechaguliwa katika timu ya wachezaji mwaka wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza.
Van Persie alikuwa ndiye mchezaji pekee wa Arsenal huku Walker akiwa ni
miongoni mwa wachezaji watatu wa Spurs katika timu hiyo huku “team mate”
wenzake wengine walioteuliwa katika timu hiyo wakiwa ni akina Scott Parker na Gareth.
Premier
League team of the year inawachezaji wengi wakiwemo akina
: Joe Hart
(Man City), Kyle Walker (Tottenham), Vincent Kompany (Man City), Fabricio Coloccini
(Newcastle), Leighton Baines (Everton), David Silva (Man City), Yaya Toure (Man
City), Gareth Bale (Tottenham), Scott Parker (Tottenham), Robin van Persie
(Arsenal), Wayne Rooney (Man Utd).
Championship team: Kelvin Davis (Southampton),
Nathaniel Clyne (Crystal Palace), James Tomkins (West Ham), Curtis Davies
(Birmingham), Ian Harte (Reading), Adam Lallana (Southampton), Peter
Whittingham (Cardiff), Mark Noble (West Ham), Matt Phillips (Blackpool), Rickie
Lambert (Southampton), Jay Rodriguez (Burnley).
League One team: Ben Hamer (Charlton), Jack Hunt
(Huddersfield), Michael Morrison (Charlton), Harry Maguire (Sheff Utd), Rhoys
Wiggins (Charlton), Johnnie Jackson (Charlton), Stephen Quinn (Sheff Utd),
Stephen Gleeson (MK Dons), Darren Potter (MK Dons), Jordan Rhodes
(Huddersfield), Ched Evans (Sheff Utd).
League Two team: Robert Olejnik (Torquay), Paul
Caddis (Swindon), Kyle McFadzean (Crawley), Ian Sharps (Shrewsbury), Kevin
Nicholson (Torquay), Matt Ritchie (Swindon), Marlon Pack (Cheltenham), Eunan O'Kane
(Torquay), Lee Mansell (Torquay), Izale McLeod (Barnet), Tyrone Barnett
(Crawley).
Angola: ASA thrash Interclube to move
fourth
Atletico
Sport Aviaçiao imefanikiwa kujisogeza mpaka kaika nafasi ya nne katika msimamo
wa ligi kuu ya nchini Angola “Angolan championship” baada ya kuichapa Interclub
kwa mabao 3-1 katika mchezo wa mzunguko wa 8 wa ligi hiyo.
Sasa Atletico
Sport Aviaçiao imejikusanyia points 15 huku Interclube wakiwa bado wanalamba
mchanga katika nafasi ya 14 wakiwa na points nne pekee.
Rotterdam Marathon race: Ethiopia win
Wanariadha
wawili raia wa Ethiopia wameshinda mbio za Marathon za Rotterdam nchini
uholanzi. Yemane Adhane kwa upande wa wanaume na Tiki Gelana upande wa wanawake
na ambaye ametengeneza rekodi mpya.
Tiki Gelana ameweka
rekodi yake mpya yam bio hizo za marathoni baada ya kutumia masaa mawili dakika
18 na sekunde hamsini na saba (2h 18 57).
Kwa upande
wa wanaume Yemane Adhane ameshinda mbio hizo akifuatiwa na raia mwingine wa Ethiopia
Getu Feleke.
Gelana
ametumia muda wa masaa mawili dakika nne na sekunde thelathini na nane (2h 04
38s).
Kumbuka
wanariadha kutoka nchini Kenya Wilson Kipsang na Mary Keitany jana walichukua
ushindi kwa kishindo katika mashindano ya Jumapili ya mbio za London Marathon
mwaka 2012.
Katika mbio
za wanaume, Kipsang aliweza kuongoza katika maili saba za mwisho, na ilikuwa
nusra avunje rekodi ya mashindano ya London.
Alimaliza
kwa muda usiokuwa rasmi wa saa 2:04.44.
Mkenya
mwenzake Martin Lel alifanikiwa kumpita mwanariadha wa Ethiopia, Tsegaye
Kebede, na ambaye ameshawahi kuwa mshindi wa mashindano ya London, na kumaliza
katika nafasi ya pili, katika kasi ya juu mno katika kumalizia mashindano.
Keitani
amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa London Marathon
Kebede,
aliyemaliza wa tatu, alifanikiwa kuwazuia Wakenya kuzoa nafasi zote tatu za
mwanzo kwa upande wa mbio za wanaume, lakini kwa upande wa kina dada juhudi za
Waethiopia hazikufanikiwa.
Hart: Title race is back on
Mlinda
mlango wa Manchester City Joe Hart anaamini kuwa kikosi chao kimerejea katika
mawindo ya taji la ligi kuu ya Uingereza baada ya kutereza kwa man united hapo
jana huku timu hizo mbili zikiwa zinzelekea katika crucial derby wiki ijayo.
Hart na kikosi
kamili cha City hapo jana waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves matokeo
ambayo amefanya touti ya alama yaani points kupungua na sasa kukiwa na tofauti
ya alama tatu na mchezo baina yao ukitazamiwa kufanyika Etihad Stadium City
wakipewa nafasi ya kufanya uzuri.
Ananukuliwa
Hart anasema
"tumekuwa
tukiangalia sana jinsi ya kumaliza msimu vizuri na tumejiweka katika nafasi
nzuri ambayo haina mashaka kuliko ilivyokuwa hukonyuma
Wakati hayo
yakiwa hivyo mzee Alex Ferguson bosi wa
united amesema anaisubiri kwa hamu hiyo inayoitwa "biggest derby" katika historia ya ufundishaji
wa soka akiwa Old Trafford licha ya
matokeo ya kushindwa kuwanyoa Everton hapo jana.
Ferguson amenukuliwa
akisema
"We need a result. Ni derby inayokuja
katika hali ya aina yake kutokana na mazingira ya kuelekea kwenye taji baina ya
timu hizo mbili pekee mahasimu wa soka katika jiji la Manchester."
Mchezo huu
unakuja wakati ambapo inakumbukwa derbi iliyopita mwezi October mwaka jana City
wakiifinyanga United kwa mabao 6-1 kikosi cha United kikiwa na wachezaji 10
uwanjani.
Man City's Mario Balotelli handed
Italy boost for Euro 2012
Kocha wa
kikosi cha timu ya taifa ya Italy Cesare Prandelli amesisitiza kuwa
mshambuliaji wa nyota wa Manchester City Mario Balotelli anasalia kuwa muhimu katika
kikosi chake kuelekea katika fainali za Euro 2012.
Ananukuliwa
Prandelli akisema
"sikuwahi
kufanya kazi bila ya Balotelli, yeye ni “focal point” katika timu ya taifa".
Senegal and Oman meet for Olympic
football berth
Senegal na Oman
zinakutana katika mchezo wa play-off hii leo kusaka nafasi ya mwisho katika
michuano ya soka ya michezo ya Olympic.
Mshindi wa
mchezo huo atakuwa anaelekea katika bakuli la draw hapo kesho.
Kocha wa
kikosi cha wachezaji wenye umri wa miaka 23 Aliou Cisse anasema
“kucheza Olympics ni muhumu zaidi ya kombe la
dunia ”
Mchezo huo
utafantika katika uwanja ulioko katika mji wa Coventry City dimba la Ricoh
Arena mmoja wa viwanja vya michezo ya Olympic.
Senegal
ilimaliza katika nafasi ya nne katika kampeni za na kupata nafasi ya play-off huku
Oman wakishinda michuano midogo ya kufuzu toka barani Asia.
Endapo
Senegal itashinda mchezo wake dhidi ya Oman itakuwa inaingia katika draw kubwa
itakayofanyika kesho katika uwanja wa Wembley na kujiunga na mataifa ya
Great
Britain, South Korea, Japan, United Arab Emirates, Gabon, Morocco, Egypt,
Mexico, Honduras, Brazil, Uruguay, New Zealand, Spain, Switzerland na Belarus
kwa upande wa timu za taifa za wanaume ilhali pia draw itakuwa ikihusisha timu
za mpira wa miguu za wanawake.
Timu za
taifa za wanawake ni pamoja na Great Britain, Japan, North Korea, South Africa,
Cameroon, United States, Canada, Brazil, Colombia, New Zealand, Sweden na France.
Yanga Yaomba Radhi Mkutano Mkuu
Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF
akiwakilisha klabu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi
wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel
Nkongo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10
mwaka huu.
Pia
alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini
iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka
sasa hawajalipa faini hiyo.
Rais Tenga
alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile. Aliongeza kuwa kwa vile yeye ni muumini
wa kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi kutoa msamaha,
hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.
Pia Rais
Tenga alisema binafsi haziingilia kamati za TFF katika uamuzi ambao zinafanya
kwa vile zina watu waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa adhabu,
angetoa adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi havikubaliki
katika mchezo wa mpira wa miguu.
Bajeti Ya Mwaka
Bajeti ya
Mwaka 2012 ya sh. 7,246,628,650 kwa ajili ya matumizi ya TFF ilipitishwa. Kwa
mwaka 2012 TFF inatarajia kukusanya sh. 7,572,991,433 kupitia vyanzo
mbalimbali.
Vyanzo hivyo
ni viingilio vya uwanjani vinavyotarajiwa kuingiza asilimia 22 ya mapato yote,
udhamini (asilimia 74) na vyanzo vingine kama haki za matangazo ya televisheni,
ada za ushiriki wa timu katika mashindano mbalimbali, misaada kutoka FIFA na
CAF ambayo kwa pamoja vinatarajiwa kuingiza asilimia nne ya mapato yote.
Marekebisho Ya Katiba
Mkutano Mkuu
wa TFF umepitisha marekebisho ya Katiba katika maeneo mawili; moja ni kuanzisha
Baraza la Wadhamini ambalo linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watatu na
wasiozidi watano.
Marekebisho
mengine ni kuongeza idadi ya kanda kutoka kumi na moja za sasa hadi 13.
Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuongeza mikoa mipya ya
kijiografia.
Kanda mpya
sasa zitakuwa Kagera/Geita, Arusha/Manyara, Kilimanjaro/Tanga, Katavi/Rukwa,
Njombe/Ruvuma, Dodoma/Singida, Dar es Salaam, Shinyanga/Simiyu, Mwanza/Mara,
Lindi/Mtwara, Kigoma/Tabora, Mbeya/Iringa na Pwani/Morogoro.
Ukiondoa
mamlaka ya uteuzi aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wote wa
Kamati ya Utendaji huchaguliwa kwa kanda.
Mfumo Wa Mashindano
Kwa vile
kuna tatizo la ligi mbalimbali kuwa fupi, hali inayosababisha baadhi ya
wachezaji katika madaraja ya chini kucheza ligi zaidi ya moja katika msimu
mmoja, mfumo wa ligi/mashindano utaangaliwa upya.
Mfumo uliopo
sasa uliwekwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika mpira wa miguu ambapo
mwekezaji anaweza kuanzisha timu, na ndani ya miaka mitatu ikacheza Ligi Kuu.
Pili, ilikuwa ni kuondoa mlolongo mrefu wa ligi, na kuwafanya wanachama wa TFF
(mikoa) nao kuendesha ligi zao mikoani.
Ijulikane
kuwa ligi za mikoa (regional leagues) zinachezwa. Kwa sababu TFF inaendeshwa
kwa mfumo wa shirikisho (federation), nia ni wanachama wa federation nao kuwa
na majukumu ya kusimamia na kuendesha ligi, kwa vile TFF haiwezi kusimamia ligi
zote.
No comments:
Post a Comment