KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 25, 2012

Harry Redknapp :England lazima isake vijana

Harry Redknapp
 Bosi wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini timu ya taifa ya Uingereza ‘Three Lions’ lazima ijenge imani kwa vijana ili iweze kuboreka na mabadiliko ya makocha yanapaswa kutazama vizazi vipya.
Redknapp anaamini England lazima endeleze vijana ili ifanikiwe katika ngazi ya kimataifa baada kuondoshwa katika fainali za Euro 2012 na Italia kwa njia ya penati.
Uingereza imeondoshwa kwa njia ya penati baada ya kuelemewa katika sehemu kubwa ya mchezo wa jana ndani ya dakika 120 na Italia maarufu kama Azzurri.
Bosi huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur anadhani chama cha soka cha Uingereza FA lazima iaangalie kizazi kipya ambao wataweza kucheza aina nyingine ya soka.
Akizungumza na The Sun amesema
"tuwalete watoto wetu wacheze wacheze. Kubali si suala la nguvu , ukubwa au haraka"
"nina matumaini makubwa na kituo kipya cha maendeleo  cha St George’s na makocha katika kila hatua nchini Uingereza.
Katika kampeni yao ya kufuzu kombe la dunia 2014 Uingereza itakuwa na safari kuifuata Moldova September 7.

No comments:

Post a Comment