Baada ya Twiga Stars kushindwa kufuzu kuelekea katika fainali za mataifa ya Afrika nchini Equtorial Guinea baadaye mwaka huu, timu za Taifa za wanawake za Nigeria, Cameroon, Cote
d’Ivoire, Ethiopia, South Africa, DR Congo na Equatorial Guinea zimefuzu fainali hizo zitakazo pigwa nchini Equtorial Guinea.
Timu ya
taifa ya wanawake wa Nigeria (Super Falcons) imefuzu fainali za mataifa
ya Afrika kwa wanawake 2012 baada ya
kuwachapa Zimbabwe 4-0 katika mchezo wa pili wa kuwania kufuzu mchezo ulipigwa Lagos
jumamosi.
Super Falcons imefanikiwa ikiwa kaida yao
kufanya hivyo tangu kuanzishwa mwaka 1998 kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-0.
Mabingwa hao watetezi walikuwa ni zaidi mara
dufu kimchezo mbele ya Mighty Warriors na kuthibitisha hadhi yao wakiongoza
mpaka kipindi cha kwanza kwa mabao matatu.
Ndani ya
dakika sita mchezaji bora wa mwaka Perpetua Nkwocha alifunga bao la uongozi kwa
shambulizi zuri kabla ya Desire Oparanozie kuongeza la pili dakika 14 baadaye.
Dakika mbili
baadaye Esther Sunday akaongeza la tatu licha
ya juhudi za mlinda mlango wa Zimbabwe Onai Chingowo kujaribu kuokoa mpira huo.
Kiungo mkongwe Stella Mbachu alimalizia karamu
kwa goli la nne kunako dakika ya 55 ya mchezo.
No comments:
Post a Comment