KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 10, 2012

Barcelona dhidi ya Real Madrid October 7

Mahasimu wakubwa katika soka la nchini Hispania watakutana kwa mara ya kwanza katika ule mchezo maarufu na mkubwa nchini Hispania ndani ya kipindi cha miezi miwili tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi hiyo katika mchezo wa kwanza utakao pigwa Camp Nou wakati ambapo mchezo wa marudiano ukipangwa kuchezwa mwezi March mwakani.
Ratiba ya ligi kuu ya Hispania maarufu kama La liga imetangazwa ikiwa ni matayarisho ya msimu mpya wa  2012-13 ambapo macho na masikio yakiwa yameelekezwa katika mchezo wa mahasimu na wapinzani wakubwa Real Madrid na Barcelona.
Blaugrana watakutana na Los Blancos October 7 na mchezo wa marudiano ukipangwa kufanyika Santiago Bernabeu March 3.
msimu huu mpya wa ligi ya Hispania unatarajiwa kumalizika August 18.
 mabingwa watetezi wa taji hilo Madrid wataanza kampeni ya kutetea taji hilo wakiwa nyumbani dhidi ya  Valencia wakati ambapo Barcelona watakuwa na kazi dhidi ya Real Sociedad nyumbani Camp Nou.

No comments:

Post a Comment