KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 13, 2012

MANJI ANGURUMA JANGWANI 'NIPENI MAJEMBE NIFANYE KAZI'





Mgombea wa nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga Yusufu Manji amefanya kampeni yake ya kwanza jioni hii akiwa na wagombea wengine wa nafasi za makamu mwenyekiti na ujumbe walio katika kambi moja Abdalah Bin Kleb, Clement Sanga na Musa Katabalo, George Manyama na Lameck Nyambaya katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kaunda makao makuu ya klabu hiyo
Manji akiwa na wapambe wake na wazee wa baraza la wazee wakiongozwa na mzee Ibrahim Akilimali wamewataka wanachama kuwachagua wao ili kuweza kuwaongoza katika kipindi cha miaka miwili ya awamu hii ya uongozi iliyosalia ili kuwaletea maendeleo wanayanga.
Manji ambaye si muongeaji sana alifika katika mkutano huo saa 11 jioni na kuwataka wanachama waliokuwa wakimsikiliza kumchagulia viongozi wenzake watakao unda kamati ya utendaji itakayo kuwa ikifanya kazi kwa vitendo na si maneno.
Amewataja wagombea anaowataka katika safu yake kuwa ni Abdalah Bin Kleb, Musa Katabalo, Clement Sanga na George Manyama ambao anaamini wataunda kamati yenye nguvu na ya maendeleo.
Awali akimtambulisha kwa wanachama waliokusanyika katika uwanja wa makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani katibu wa baraza la wazee Ibrahim Akilimali amesema ni wagombea hao ndio waliompa jeuri ya kusema anazo shilingi milioni 750 kwa lengo kuuondosha na kuubomoa uongozi uliopita chini ya aliyekuwa kwenyekiti wakati huo Loyd Nchunga.
Akilimali amesema katika zoezi la kuomba kura wagombea hao hawatapata nafasi ya kutembelea matawi yote hivyo basi matawi ambayo yatapata nafasi ya kutembelewa na wagombea hao ni Makangarawe  ,Kigamboni na Kawe.
Akilimali amewataka wagombea wamuunge mkono Yusufu Manji na wagombea wengine wa safu ambayo ameipendekeza yeye Manji ili waweze kuleta maendelea ndani ya klabu hiyo.
Kwa upande wake Abdalah Bin Kleb mgombea wa nafasi ya ujumbe amewataka radhi wanachama huko katika matawi kwa kushindwa kutokea kwenye kampeni kwasababu alikuwa bize na usajili lakini amesema akipata uongozi atapita matawini kwa ajili ya kuwashukuru.
Manji pia amesema anajua wanaingia kwenye uchaguzi huku wakiwa na deni la mabao matano waliyofungwa na wapinzani wao wa jadi Simba na kwamba deni hilo litalipwa watakapo kuwa katika uongozi.
Pia  amesema hataweza kusema sera zake kwa kuwa wanachama wanajua ni nini wanataka lakini atafanya kwa vitendo na si maneno huku akitumia maneno nipeni vitendea kazi nifanye kazi

No comments:

Post a Comment