KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 13, 2012

BREAKING NEWS:UCHAGUZI YANGA,WAKILI TASLIMA ATAKA UCHAGUZI UHAIRISHWE

Taslima law chambers advocate imemwandikia barua katibu mkuu wa yanga ikitaka mkutano wa uchaguzi uhairishwe kwasababu ni batili kwa kuwa katiba halali ya yanga ni ile ya mwaka 1968 na si nyingine.
Barua imesema kuna wanachama wa kadi ya katiba ya mwaka 1968 watakosa haki yao ya kikatiba ya kushirikia uchaguzi kwasababu majina yao hayajaorodheshwa katika orodha baada ya katiba ya sasa kutengenezwa .
Barua hiyo imetoa rai kuwa uchaguzi huo uhairishwe ili kuepusha matatizo ya kisheria yanayo weza kutokea na kunyima kutoa nafasi kulitatua suala hilo.
Barua hiyo imesainiwa na na Taslima wakili wa Taslima Law Chambers na nakala mbalimbali kusambazwa kwa mwenyekiti wa DRFA , msajili wa vyama vya michezo na katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF.
Barua hiyo imesema usajili wa wadhamini ambao  ni trusteeship kama Yanga unafanyika kisheria chini ya sheria ya the Trustees incorporation Act (cap318R.200) na si vinginevyo .
Ofisi ya mrajisi mkuu tayari imeshaelekeza kimaandishi kuwa wanatambua wadhamini waliotokana na katiba ya mwaka 1968 tu.
Kuna uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu ya tarehe 1/07/2010 kwenye shauri la madai no 98 la 2010 unaelekeza kuwa uchaguzi wowote utafanyika Yanga uzingatie katiba ya mwaka 1968 hivyo uchaguzi wowote utafanyika bila kuzingatia katiba hiyo ni batili

No comments:

Post a Comment