Diego
Maradona amepaza sauti yake akitoa maoni yake kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo hataweza kufikia kiwango alicho nacho mshambuliaji wa Barcelona Lionel
Messi.
Washambuliaji
wote wawili wanaonekana kuwa katika nafasi sawa ya kushinda tuzo ya FIFA ya Ballon
d'Orbaada ya kuwa na msimu mzuri lakini bado Maradona anadhani Mreno hamkaribii
kabisa kiuwezo Muajentina.
Amenukuliwa akisema
"Cristiano
Ronaldo hawezi kuwa katika kiwango kama alichonacho Messi. Lionel haitaji nguvu
za kupiga alizonazo Cristiano Ronaldo. Messi yeye ana dribble yaani anakokota
mpira kuelekea golini akiwa na mpira wake mguuni," Maradona alikuwa
akiongea na TVR.
Katika hatua
nyingine muwasisi huyo wa jezi No.10 duniani alikuwa na maoni tofauti juu ya
michuano ya ulaya ambapo aliandika juu ya Ronaldo ambapo alinukuliwa akisema Ronaldo
ni mchezaji bora kama ilivyo kwa Lionel Messi, akichanganywa na aina ya
uchezaji wake alipokuwa akiitumikia Ureno katika michuano hiyo
Katika hatua
nyingine nyota huyo wa michuano ya kombe la dunia 1986 alichukizwa na
kulinganishwa na Messi.
Amenukuliwa akisema
"sipendi
kulinganishwa naye .lakini kunilinganisha naye ni kitu kizuri sisi wote
tunatumia miguu ya kushoto,wote tuna toka Argentine na tunang’ara"
No comments:
Post a Comment