KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 14, 2012

Timu ya Al Salaam Wau ya sudan kusini hovyo yabanjuliwa 7-0 na APR katika michuano ya vilabu ya Cecafa


Al Salaam Wau klabu bingwa ya Saudan Kusini hii leo imenja tamu na chungu ya michuano ya Kagame baada ya kuchapwa jumla ya mbao 7-0 na APR ya Rwanda mchezo wa kwanza na wa ufunguzi wa michuano ulipigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa michuano ya mwaka huu lakini pia ni mchezo wa kwanza klabu bingwa ya kusini kusini kushiriki tangu kujiunga na michuano hiyo nchi ambayo ilipata uhuru wake wa kwanza jumatatu iliyopita.
Katika sehemu ya shamra shamra ya uhuru wan chi hiyo kulikuwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa ambapo 'Bright Star' ilikwenda sare ya bao 2-2
    Group A: Simba (Tanzania), URA (Uganda), AS Vita Club (DR Congo), Ports (Djibouti)
    Group B: Azam (Tanzania), Mafunzo (Zanzibar), Tusker (Kenya)
    Group C: Yanga (Tanzania), APR (Rwanda), Al Salaam Wau (South Sudan), Atletico (Burundi)
Licha ya kupata kichapo hicho kocha wa Al Salaam's Mel Yok Kuol alionekana mwenye furaha na kiwango cha wachezaji wake.
APR ilipata mabao yake matatu katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Lionel St Preus, Jean Baptist Mugireneza na mkongwe Olivier Karekezi.
St Preus akaandika bao la pili kipindi cha pili huku Seleman Ndikumana akiandika bao linguine kabla ya Barnabe Mubumbyi akiandika bao la saba.
Licha ya kuwa wepesi wa kupoteza mpira Al Salaam walikuwa na nafasi za kutengeneza nafasi za kufunga laikini ugeni katika michuano ilikuwa ni kikwazo kwa maana ya kukosa uzoefu.
Nafasi nzuri ilipotezwa na nahodha Khamis Leon dakika ya 60 ambapo mpira wake ulikwenda moja kwa moja kwa mlinda mlango wa APR Jean Claude Ndoli.
Kocha wa Al Salaam Sebit Bol Chol amekiri wachezaji wake kukosa uzoefu.

No comments:

Post a Comment