KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 7, 2012

EMMANUEL OKWI:SIONDOKI SIMBA NG'OO


Mshambukliaji wa simba Emmanuel okwi amekanusha taarifa za kuwa yuko mboni kuelekea katika klabu ya Yanga akisema taarifa hizo zilikuwa ni uzushi mtupu.

Okwi amesema ameshangazwa na taarifa kuwa huenda akaelekea katika klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es salaam.
Akiongea na Rockersports akiwa tayari yuko jijini Dar es salaam amesema yeye hana mpango wowote wa kuelekea kucheza soka katika klabu ya Yanga na kwamba bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Saimba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
Okwi amekanusha juu ya kukutana na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Abdalah Bin Kleb huko katika jiji la Kampala nchini Uganda akisema taarifa hizo amezisikia alipofika jijini Dar es salaam.
Kuhusu taarifa za majaribio yake nchini Austria katika klabu ya fc Salzburg amesema yamekwenda vizuri na kilicho mrudisha nyumbani Afrika ni kutokana na kupatwa na malaria ambayo alilazimika kujitibia nchini Uganda.
Kuhusu hatma yake ya baadaye katika soka amesema yeye ni mchezaji halali wa Simba na atakuwepo katika tamasha maarufu la klabu hiyo maarufu kama Simba Day isipokuwa hatakuwepo uwanjani kwa kuwa bado ana sumbuliwa na malaria.

Rockersports pia ilibahatika kuongea na makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu ambaye amesema wamefurahishwa na kuwasili kwa Okwi na kwamba atatambulishwa kwa wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kama itakavyokuwa kwa wachezaji wengine katika uwanja wa Taifa kabla ya mchezo dhidi ya Nairobi City Stars ambao ni kuhitimisha sherehe ya Simba Day.

1 comment:

  1. akifeli majaribio ndio hivyo tena atakuwa amebakiza mwaka mmoja amba ikibaki miezi sita atakuwa huru kuzungumza na timu yoyote na kama muda huo ukimalizika atakapopata timu simba haitaambulia hata senti tano,habari ndiyo hiyo

    ReplyDelete