KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 24, 2012

KIMATAIFA: Mourinho anasema goli la kwanza la Barcelona la off-side,Alexandre Song-Nataka kushinda mataji nikiwa na Barcelona na Marcelo anasema Supercopa ni mali ya Madrid.


 Mourinho:Goli la kwanza la Barcelona la off-side.

Jose Mourinho na Tito Vilanova wakipeana mikono baada ya mchezo kumalizika
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anaamini kuwa mwamuzi wa pembeni alifanya kosa kubwa kwa kuruhusu goli la Pedro na kupelekea mchezo kumalizika kwa matokeo ya timu yake kuchapwa mabao  3-2 na Barcelona katika mchezo wa kwanza wa Supercopa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania alifunga goli la kusawazisha la Barca kunako dakika ya 56 baada ya baada ya kumzidi Fabio Coentrao, lakini kupitia luninga ilionekana kuwa alikuwa tayari amejenga kibanda yaani ameotea.
Amenukuliwa Mourinho akisema
“goli la kwanza la Barcelona lilikuwa ni makosa ya mwamuzi na ndivyo ilivyo,”
Kocha huyo raia wa Ureno ameelezea juu ya uwezo wa kikosi chake ikiwa ni pamoja na kumpongeza winga wake Jose Callejon.

“si kupenda kipindi cha kwanza kilivyokuwa lakini katika kipindi cha pili mambo yalikuwa tofauti. Callejon alicheza vizuri. Alimuandalia mazingira mazuri kimchezo Di Maria. Huu uilikuwa ni mchezo muhimu nimependa kazi yakek,”
Katika mchezo wa pili Supercopa itahamia Santiago Bernabeu baada ya siku sita, lakini pia timu zote hizo zitakuwa katika michezo ya ligi ya Hispania La Liga mwishoni mwa juma ambapo Madrid watakuwa na kibarua dhidi ya Getafe na Barcelona dhidi ya Osasuna.


Marcelo: Supercopa ni kama imekwisha 

Marcelo
Mlinzi wa kushoto wa kimataifa wa Brazil na Real Madrid Marcelo anaamini taji la Supercopa litakwenda Bernabeu lakini pia akifurahishwa na mchezo ulioonyeshwa na Madrid dhidi ya Barcelona.
Akiongea na TVE baada ya mchezo huo Clasico uliomalizika kwa Madrid kuchapwa mabao 3-2 kule Camp Nou,mlinzi huyo wa pembeni amefarijika na kiwango cha  Los Blancos na anaamini kikosi chake kinafaida ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa wa marudiano.


Alexandre Song-Nataka kushinda mataji na Barcelona



 Kiungo mpya wa Barcelona Alexandre Song amesema anatamani kutwaa mataji na kufanya vizuri akiwa ndani ya jezi ya blaugrana baada ya kusaini katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Arsenal.
Akiongea kupitia mtandao wa klabu yake amesema anajisikia fahari kuwa ni sehemu ya kikosi cha Tito Vilanova ambacho kinacheza  'tiki-taka' style.
Kiungo huyo wa kimataifa wa ambaye anacheza kama kiungo mkabaji ameweka wazi matarajio yake kuwa atakuwa kwenye kipindi cha mafanikio chini ya kocha wake mpya Vilanova.
Song ambaye amekabidhiwa jezi nambari  No. 25 amemzungumzia rafiki yake wa karibu toka wakiwa wote  Arsenal Cesc Fabregas kuwa ndiye chagizo la kumfanya acheze mpira mzuri Camp Nou.
Song anaamini kuwa atafanikiwa kuhimili kipindi hiki kigumu cha mpito cha kutoka kwenye soka la English mpaka Hispania na anadhani uwezo wake na fitness yake itajihirisha kuwa ni azina kubwa ndani ya Camp Nou.
"niko vizuri katika mazingira ya mtu na mtu kwa kawaida huwa najaribu kuupata mpira. Nafikiri mpira wa kingereza na Hispania kuna tofauti kidogo. Uingereza ni nguvu kidogo tofauti na hapa hivyo napaswa kuiga. Sidhani kama aina yangu ya mchezo itabadilika lakini nitalazimika kuwa vizuri zaidi”

No comments:

Post a Comment