KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 23, 2012

Soma kimataifa :Adebayor anategemea mambo mazuri na Tottenham msimu huu,Leonardo:Messi & Cristiano Ronaldo si lolote si chochote kwa Ibrahimovic,Giggs: usajili wa RVP ni ujumbe na Stramaccioni amwagia sifa kwa Zaneti akimuita 'bionic' .


Adebayor anategemea mambo mazuri na Tottenham msimu huu
Mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor ametanabaisha kuwa anategemea kuwepo katika kipindi kizuri cha kudumu katika klabu yake hiyo baada ya mpango wa kudumu kukamilika.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amefanikiwa kupata mkataba wa kudumu kwa gharama ya pauni milioni £5 toka Manchester City wiki hii na anamatumaini ya kujenga zaidi uwezo wake wa kufumania nyavu zaidi ya magoli 18 aliyofunga msimu uliopita pale White Hart Lane.
Adebayor alikuwa ni sehemu muhimu katika kikosi cha Harry Redknapp ambacho ilikuwa kidogo kucheza vilabu bingwa Ulaya kutokana na Chelsea kutwaa taji la Ulaya mwezi May.
Amenukuliwa Adebayor akisema,
"mwaka uliopita nilikuwa katika kipindi kigumu , na hiyo ndio sababu kila mchezo msimu huu utakuwa mgumu kama ulivyoona mchezo wa jumamosi. Newcastle walikuwa na timu nzuri.
"Manchester United, Manchester City, Chelsea, Arsenal, Tottenham na Newcastle watakuwa katika vita ya kuwania nafasi za juu nne.
"haitakuwa rahisi, lakini kama mcheza soka unapaswa kufanya mambo yako na kuangalia nini kimetokea mwisho wa msimu."
Mambo ya kifedha yalimchelewesha Adebayor kupata mkataba wa kudumu kule kaskazini mwa London toka Manchester City na mshambuliaji huyo raia wa Togo amefurahia kupata mkataba huo.
 
Leonardo:Messi & Cristiano Ronaldo si lolote si chochote kwa Ibrahimovic.
Mkurugenzi wa soka wa Paris Saint-Germain Leonardo anadhani hakutakuwa na mshambuliaji bora kuliko Zlatan Ibrahimovic, na kusisitiza kuwa MSwedish huyo hawezi kulinganishwa na Lionel Messi au Cristiano Ronaldo.
amenukuliwa na L’Equipe Leornado akisema
"tunaweza kuwazungumzia Messi na Cristiano Ronaldo, lakini si lolote kwa  Ibrahimovic. kwa kilo 100 na mita  1.96 ni bora katika kufumania nyavu duniani ,"
"wakati tunamsaini  Thiago Silva na Zlatan msimu huu kila mtu alivutiwa na kile tulicho kifanya baada ya miaka miwili au mitatu watu watakuwa na majibu sahihi juu ya utoufauti tunaousema"
Mbrazil huyo amesisitiza kuwa wameweka offer nyingine kwa ajili ya mlinzi wa Lille ya Ufaransa  Mathieu Debuchy.
amesema,
"ni mchezaji mkubwa na ni mchezaji wa wakala huyo huyo wa Mathieu Bodmer,kwa hiyo unaweza kusema kuwa tumesha kuwa karibu naye. hatukuwahi huko nyuma kuzungumzia hili .."
PSG imekuwa katika jitihada ya kutafuta kiwango bora katika wiki za mwanzo wa kununua wachezaji msimu huu lakini Leonardo amekuwa hana mashaka juu ya zoezi hilo.
Paris Saint-Germain inatarajia kufungua msimu mpya wa ligi ya Ufaransa “Ligue 1” kwa ngarambe itakayopigwa pigwa jumapili dhidi ya Bordeaux.
Giggs: usajili wa RVP ni ujumbe
 Usajili wa Manchester United kwa Robin van Persie toka Arsenal ni ujumbe mkubwa kuwa klabu hiyo inataka kuchukua mataji msimu huu, hii ikiwa ni kauli ya mkongwe  Ryan Giggs.
Van Persie alijunga na Old Trafford toka Emirates kwa ada ya pauni milioni £24 baada ya msimu wa tetesi kubwa kuwa alikuwa na mpango wa kuaelekea katika vilabu kadhaa ikiwepo Manchester City na Juventus.
Mkongwe Giggs anasema United ilikuwa imejipanga kufunika machungu yake ya kukosa taji msimu uliopita kwa utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa na kumaliza msimu uliopita mikono mitupu nyuma ya City.
amenukuliwa Giggs kupitia mtandao wa United akisema  
"Usajili wa Van Persie ni ujumbe mkubwa, ni jambo kubwa kwa mchezaji kuja hapa na kusema alikuwa anataka  kuja katika klabu hii.
"Najipendelea lakini wachezaji wanapaswa kuwa na utashi wa kuja United kwasababu tuna kawaida ya kuwa na  “guaranteed” ya kutwaa mataji hiyo ndiyo ‘spirit’ yetu na unapata nafasi ya kufundishwa na meneja mkubwa . kuna mengi yakujivunia."
 Muller: Bundesliga itakuwa ni timu mbili Bayern na Dortmund
Thomas Muller haoni sababu kwa nini mbio za taji la soka nchini Ujerumani isiwe ya vilabu Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anadhani timu nyingine zinaweza kuingia katika mbio hizo za taji tangu mapema kwa msimu lakini akaongeza kuwa ni BVB na Bayern zinazoweza kuwa katika changamoto ya taji mpaka kumalizika kwa msimu.
amenukuwa kupitia mtandao wa klabu akisema
"unaweza kuziona timu nyingine nyingi katika mbio lakini kimsingi nadhani Bayern na Dortmund ni timu mbili zenye ubora na uwezo katika kipindi chote ".
Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa pia amezungumzia juu ya mchezo wa ufunguzi mwishoni mwa juma wa ligi kuu ya nchini Ujerumani Bundesliga dhidi ya Greuther Furth akisema timu hiyo mpya haita kuwa daraja.
"utakuwa ni mchezo mgumu ,Furth iko katika kiwango kizuri hasa baada ya kupata nafasi ya kujiweka vizuri kimaandalizi na wanaweza wakaendeleza historia yao nzuri ya kufanya vizuri katika uwanja wao wa nyumbani,".
Stramaccioni amwagia sifa  kwa Zaneti akimuita 'bionic'
Kocha wa Inter Milan Andrea Stramaccioni amesema nahodha wake Javier Zanetti ni sawa na "bionic" yaani kifaa ambacho kinamsaidia mwanadamu kufanya kazi kuwa rahisi wakati huu ambapo mchezaji huyo akiwa katika maandalizi ya kukamilisha mchezo wake wa 800th ndani ya klabu hiyo hii leo.
Stramaccioni amenukuliwa akisema  Zanetti ambaye kwasasa ana umri wa miaka 39, "is not human".
Ametoa kauli hiyo kwa waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa kuwanuia kufuzu michuano ya Europa League dhidi ya Vaslui ya Romania.
Kioungo huyo raia wa Argentina alijiunga na Inter mwaka 1995,na kukamilisha jumla ya michezo 700 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa mwaka 2010 mchezo ambao Inter Milan iliichapa Bayern Munich mabao 2-0 kule Bernabeu.
Stramaccioni ambaye kiumri ni mdogo kwa utofauti wa miaka mitatu amenukuliwa akisema
"ni kitu cha kipekee . sikuwahi kufikiri  au kuona mtu anacheza michezo 800 katika maisha yangu yote . nahodha wangu lazima atakuwa ‘cloned’ yaani mtu wa tofauti ."
Zanetti pia anashikilia rekodi ya kucheza michezo mingi katika timu ya taifa ya Argentina akicheza michezo 145 na kucheza michezo zaidi ya 1,000  katika career hii.
 

No comments:

Post a Comment