KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 12, 2012

KIMATAIFA:Fifa yaanza tena kumchunguza Mohamed bin Hammam na nyinginezo.,

Fifa yaanza tena kumchunguza Mohamed bin Hammam
Mohamed Bin Hammam
Bodi ya utawala ya shirikisho la soka duniani fifa imeanza tena kumchunguza Rais wa zamani wa shirikisho la soka barani Asia Mohammed Bin Hamman juu ya uvunjifu wa sheria za shirikisho hilo
Qatari ilifungiwa kutokujishulisha na mambo ya soka kwa siku 90 kuanzia July 26 2012 baada ya kuonekana kufanya vitendo vilivyo fanana na rushwa katika mpango wao wa kusaka nafasi ya Urais wa Fifa mwaka 2010.
Hapo kabla Bin Hammam alipewa adhabu ya kutokujishulisha na soka maisha kabla ya adhabu hiyo kutengeliwa na mahakama ya usuluhishi ya michezo CAS July 19 kufuatia kukosekana ushahidi uliojitosheleza.
Bin Hammam alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Sepp Blatter katika kampeni za urais wa fifa na alikuwa akifanya kampeni ya gharama kubwa kumng’oa Baltter akitumia ndege binafsi lakini baadaye katuhumiwa kufanya kampeni chafu.
 Kwasasa kinachoonekana kuwa ni tatizo kwake ni uwezekano mkubwa wa kupata za kura ya kuandaa michuano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Di Matteo anasema  Manchester City & United wako mbele zaidi ya Chelsea licha ya matumizi makubwa ya usajili kiangazi.
Roberto Di Matteo
Meneja wa Chelsea Roberto Di Matteo amekubali kuwa timu ambazo zimekuwa zikionekana kwenye nafasi ya kutwaa taji msimu ujao wa ligi ya uingereza Manchester City na Manchester United bado ziko mbele ya Chelsea licha ya ‘the Blues’ kufanya usajili kwa mapesa mengi.
Mtaliano huyo ameweka wazi kuwa viungo washambuliaji Eden Hazard, Marko Marin na Oscar katika kikosi chake msimu huu wameigharimu klabu yake pauni milioni £65.
Chelsea inatarajia kucheza katika mchezo wa ngao ya jamii “Community Shield” jumapili hii dhidi ya Manchester City na Di Matteo ametabiri kuwa watadhihirisha kuwa wako vizuri.
"Manchester City ni mabingwa wa msimu uliopita, lakini tutawafunga hata kama United ndiyo inayoonekana kuwa nyuma yao kiubora.
Wakati Chelsea ikielekea katika ufunguzi wa pazi la ligi kuu ya Uingereza, pia klabu hiyo itakuwa ikiingia katika msimu mpya wa kimashindano katika michuano ya Uefa Super Cup na Fifa Club World Cup ikiwa ni kufuatia kupata mataji ya FA Cup na klabu bingwa.
Di Matteo anasema wanapaswa kupigania mataji mengine lakini kikosi chake kuongeza jitihada katika ligi kuu msimu kufuatia kumaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita 2011-12.
Manchester United itaendelea kuwekeza kwa wachezaji anasema mtendaji mkuu David Gill

Mtendaji mkuu wa Manchester United David Gill amewatetea wamilikiwa klabu hiyo na kusisitiza kuwa wanaelewa umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika wachezaji.
Gill amesema hayo kufuatia United kuweka sokoni hisa zake katika soko la New York Stock Exchange kujaribu kupata pesa zaidi ili kupunguza deni linalo ongezea Old Trafford.
Licha ya kwamba hilo bado halija fanikiwa kama United inavyo tumainia , Gill amesisistiza kuwa mfumo wa kifedha uliopo kartika klabu hiyo unaonyesha kuwa klabu hiyo itaendelea kutumia pesa zake katika kuimarisha kikosi.
 Amenukuliwa akisema
"tunafahamu na wamiliki wanaelewa kuwa kinachotokea uwanjani ni muhimu sana kwetu na tutafanya kila linalowezekana pesa inatumika kuwekeza katika timu ili tusonge mbele".
 akizungumzia wamiliki wa Glazer family amesema
"ukubwa wa deni tulilo ingia huko nyuma tangu wachukue klabu halina madhara kwa timu” .
Mtendaji huo ameendelea kusema kuwa mafanikio ya klabu hiyo katika Premier League na Champions League pamoja na makubaliano ya udhamini wa jezi na na kampuni ya Chevrolet ni katika jitihada za kuendeleza kutafuta pesa bila kujali deni la klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment