Cristiano Ronaldo kukutana
na Rais wa Real Madrid Florentino hii leo
Cristiano Ronaldo anatarajiwa kukutana na Rais wa
Real Madrid Florentino Perez hii leo kujaribu kuzungumzia juu ya hali ya mambo
ndani ya mabingwa hao wa Liga.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno aliweka
wazi wakati wa kipindi kif kuwa hana raha na masha yake ndani na Santiago Bernabeu
kutokana na sababu alizo ziita sababu za kukosekana kiutaaalam kiasi kusemwa
mengi juu ya hali yake hiyo ya kutokakuwa na furaha.
Ronaldo alirejea Madrid hapo jana baada ya
kumaliza majukumu ya kitaifa akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno ambapo mara
baada ya kurejea alikutana ana kwa ana na kocha Jose Mourinho wakiwa katika
mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa mazoezi.
Sasa anatarajiwa kukutana na Perez , ili kuweka
wazi yanayo msibu wakati Madrid ikisaka suluhisho la tatizo la mshambulizi
huyo.
FA yaomba radhi juu ya
janga la Hillsborough
Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Engalnd David
Bernstein ameomba radhi kufuatia maafa yaliyotokea Hillsborough.
Mashabiki wa Liverpool wamekuwa wakitoa heshima
zao na kutoa maua ambayo yamekuwa yakipelekwa katika uwanja wa klabu hiyo Anfield.
Maneno ya kuomba radhi yamekuja kufuatia kundi la mashabiki wa klabu hiyo linalo tambulika kama ‘Hillsborough
Family Support Group’ kutaka bodi ya utawala ya chama cha soka cha England
kuomba radhi.
FA iliruhusu mchezo wa nusu fainali wa kombe la FA
mwaka 1989 ufanyike ambapo jumla ya watu 96 walipoteza maisha katika uwanja wa Sheffield
licha ya kuwa kulikuwa hakuna kibali cha kuruhusu mchezo huo kufanyika katika
uwanja huo ambao ujaa maelfu ya watazamaji kiasi kuleta madhara makubwa.
"Tunaomba radhi kwa janga hili kutokea katika
uwanja ambao FA iliuteua. Mchezo huu ulichezwa katika michuano ambayo
inaandaliwa na FA yenyewe, kwa niaba ya FA , ninaomba radhi na tungependa kutoa
rambirambi kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao na kila mtu anae
ungana na mji wa Liverpool na klabu ya Liverpool yenyewe ".
"Hili halita tokea tena. Hakuna mtu atakae
poteza maisha atakapo kuwa amekaa akiangalia mpira , na ni suala la kujutia na
huzuni kubwa imetokea siku nyingi zilizopita na waliopoteza maisha kutambulika
na ukweli kuzungumzwa."
Mapema hii leo, FA ilitoa taarifa ambayo ilihusu
machapisho ya ripoti ya uchunguzi ya janga hilo iliyo tambulika kama ‘Hillsborough
Independent Panel's report’ ambayo ilisema kuwa janga la janga kubwa ambalo
halitasahaulika ambalo lilitokea April 15, 1989.
No comments:
Post a Comment