KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 17, 2012

THOM SAINTFIET ALALAMIKIA UONGOZI KWA KUWAPA MALAZI MABOVU MBEYA, KESHO KWENDA MOROGORO KUWAKABILI MTIBWA.


Kocha mkuu wa mabingwa wa kombe la Kagame Yanga Thom Saintfiet amesema hakuridhishwa na matokeo ya mchezo wake wa ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya ambao walikwenda sare ya bila kufungana.

Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yalioko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani hii leo amesema hakuridhishwa na matokeo hayo kwa kuwa alikwenda mbeya kushinda kama ilivyo dhamira yake ya kushinda kila mechi ili kutwaa taji la ligi kuu msimu wa 2012/2013.


Pia amelalamikia sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Sokoine kwani wachezaji wake walishindwa kuuzoea katika kipindi cha kwanza tofauti na wenyeji ambao walionekana kutawala katika kipindi hicho licha ya kwamba kipindi cha pili walifanikiwa kubadilika kimchezo.


Saintfiet amesema tatizo lingine ni kuwa katika mchezo huo Tanzania Prisons walikuwa wakicheza mchezo wa rafu kiasi kuwanyima nafasi wachezaji wake kucheza kwa kufuata maelekezo yake.


Kocha huyo ameulalamikia uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kuweka mazingira mazuri ya ushindi tangu nje ya uwanja kwani timu ilifikia katika hoteli mbaya ambayo hajawahi kuiona kote Afrika ya Peter Safari Hotel.
amesema ndani ya Hoteli hiyo wachezaji wake walilala wawili wawili huku wakikumbatiana na pia vitanda vilikuwa vibovu.
mbali na hilo huduma ya chakula haikuwa yakuridhisha kwani mbali ya ubovu wa chakula chenyewe lakini pia kilikuwa kidogo kisicho tosheleza kwa mchezaji.
sambamba na hilo huduma ya maji na vyoo ilikuwa mbaya jambo ambalo kisaikolojia linaathiri uwezo wa mchezaji katika maandalizi ya mchezo. 


Ndani ya uwanja amesema hawezi kumlaumu sana mwamuzi kwa kuchezesha mchezo vibaya bali lawama zake nyingi anazielekeza kwa uongozi kushindwa kuandaa mazingira mazuri nje ya uwanja.


Amesema uongozi wa klabu hiyo umeshindwa kumuuliza kikosi kifikie sehemu gani na nini mahitaji ya wachezaji wake jambo ambalo inawezekana wachezaji wake hawakufikia kiwango kutokana na malazi mabovu waliyokuwa wameyapata.


Tayari amekwisha kutoa taarifa katika uongozi wa yanga juu ya malazi na maandalizi ya mchezo kule Mbeya.
Yanga inaelekea Morogoro kesho asubuhi kukabiliana na Mtibwa Sugar mchezo utakao pigwa Jumatano katika uwanja Jamhuri ikiwa na jumla ya wachezaji 18 bila ya kiungo Rashidi Gumbo ambaye ni majeruhi.


Kocha huyo amesema anatarajia huo utakuwa ni mchezo mzuri japokuwa wanakwenda kucheza kwenye uwanja usiokuwa na hadhi kwao lakini hawana jinsi na wanaelekea huko kwa lengo la kupata ushindi na amesema huenda akakifanyia mabadiliko kikosi chake.
Amesema Yanga ndio mabingwa wapya wa ligi kuu msimu huu licha ya kuanza kwa sare kwani hata katika michuano ya Kagame walianza kwa kufungwa lakini walifanikiwa kutwaa taji hilo.

No comments:

Post a Comment