KOCHA
Mkuu wa timu ya taifa, ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen, ametangaza kikosi
cha wachezaji 22 watakaoingia kambini jijini Mwanza,kujiandaa na
michuano ya Kombe la Chalenji na mechi ya Kimataifa dhidi ya Harambee
Stars ya Kenya.
Katika kikosi hicho wachezaji wakongwe ni kipa Juma
Kaseja,Ngassa,Aggrey Moris na Chuji, Nyoni, Shaaban Nditi,Amir Maftaha,
Amri Kiemba, Yondani na Nasso Cholo
Akitangaza kikosi
hicho mbele ya waandishi wa habari katika Hoteli ya La Kairo jijini Mwanza ,Poulsen alisema kuwa ametumia vigezo vitatu kwa ajili ya kupata
wachezaji hao ambavyo ni vipaji, hamasa ya mchezji juu ya kuichezea timu
yake ya taifa pamoja na nidhamu na kujituma uwanjani na kueleza kuwa
katika kikosi hicho ametoa nafasi zaidi kwa vijana.
Alisema miezi sita iliyopita alichagua wachezaji makinda
Frank Domayo na Simon Msuva na kitendo kilicho washangaza wananchi
kutokana na uteuzi huo.
“Uteuzi
wangu wa wachezaji vijana chipukizi, Frank Domayo na Simon Msuva, miezi
sita iliyopita uliwashangaza wanachi, lakini vijana hao leo hii wanacheza
mpira wa uhakika,”alisema Polsen
Aliwatetea vijana aliowateuwa katika kikosi hicho akisema
anamini vijana watafanya vyema katika mechi zinazoikabili Stars na
watakuwa hazina ya nchi hii siku zijazona kuomba wapewe ushirkiano kwa
kuwapa nafasi ya kuitumikia timu ya Taifa.
Poulsen alisema amewaacha baadhi ya wachezaji kutokana na
kuwa majeruhi,huku wengine viwango vyao vikiwa vimeshuka na wengine
kufungiwa na timu zao kutokana na makosa mbalimbali.
Amesema mshambuliaji
wa Yanga Said Bahanuzi ameachwa kwa sababu ya majeruhi, huku Ramadhani Chombo Redondo,akiachwa kwa kushuka kiwango chake pamoja na Haruna Moshi
aliyefungiwa na klabu yaker ya Simba kwa utovu wa nidhamu.
Aliwataja wachezaji aliowateuwa kwa nafasi ya golikipa Juma
Kaseja (Simba)na Deogratius Munish (AZam). Mabekini Nassor Masoud
Cholo, Aggrey na Morris Erasto Nyoni (Azam) Kelvin Yondan (Yanga), Shomari
Kapombe na Amir Mafutah (Simba) pamoja na Issa Rashid.
Viungo ni Ramadhan Singano, Salum Abubakar (Azam), Athuman
Idd 'chuji, Frank Domayo (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa), Amir Kiemba
Mwinyi Kazimoto pamoja na Mrisho Ngassa (Simba).
Poulsen
amewaita washambuliaji John Boko(Azam), Simon Msuva (Yanga), Mbwana
Samata, Thomas Ulimwengu(TP Mazembe) pamoja na Edward Christopher (Simba).
Amesema kuwa timu hiyo inatarajia kuingia kambini Jumapili ya wiki hii na itakuwa ikifanyia mazoezi katika uwanja wa michezo waCCM Kirumba.
Amesema kuwa timu hiyo inatarajia kuingia kambini Jumapili ya wiki hii na itakuwa ikifanyia mazoezi katika uwanja wa michezo waCCM Kirumba.
No comments:
Post a Comment