Mshike mshike wa Ligi kuu ya
soka Tanzania bara umeendelea tena hii leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika
viwanja vitatu tofauti.
Kule Manungu
Mtibwa sugar baada ya kuichapa Simba katika mchezo uliopita hii kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kuichapa JKT Ruvu kwa bao 1-0 matokeo ambayo
yameifanya Mtibwa kufikisha jumla ya
alama 19.
Matokeo ya ushindi kwa Mtibwa hii leo yanaonyesha wazi kuwa mwendo wa Mtibwa katika ligi sasa unaridhisha, kwani wametengeneza tofauti ya alama 7 tu na kinara wa ligi hiyo Yanga wenye alama 26 jambo ambalo linaweza kuifanya Mtibwa kuwa ni miongoni mwa timu tano katika ligi kuu zenye mbio sawa katika mbio za taji.
Azam FC
imezinduka hii leo baada ya kichapo cha mabao 2-0 toka kwa Yanga jumapili iliyopita na walikuwa wakicheza dhidi ya JKT Oljoro mchezo ulifanyika
katika uwanja wa Azam Complex ambapo Azam imefanikiwa kuichapa Oljoro kwa bao
1-0 bao la Kipre Tcheche.
Nao Coast
wakiwa katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga wamefanikiwa kuichapa Polisi
Morogoro kwa bao 1-0 matokeo ambayo yameifanya timu hiyo kujiweka katika nafasi
ya nne katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 22 alama ambazo zinaifanya timu hiyo kuwa vizuri katika msimamo wa ligi ikiwa imezidiwa alama nne na Yanga wanaongoza ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment