Chelsea inabidi tuimarishe eneo letu la ulinzi anasema Ivanovic.
Mlinzi wa Chelsea
Branislav Ivanovic amesema kikosi chao kinatakiwa kuboresha eneo la ulinzi
endapo kitakuwa kinataka kuendelea kutetea taji lao la vilabu bingwa ulaya.
"kama
tunataka kufikia mafanikio tunapaswa kuwa na ukuta mgumu, hiyo ndiyo
sehemu ya kikosi chetu tunapaswa kuimarisha. Naamini tunaweza kutengeneza nafasi
dhidi ya timu yoyote na tunaweza kufunga magoli."
Mlinzi huyo wa
kimataifa wa Serbia anaamini majibu ya kwanini Chelsea inaboronga ni katika
sehemu ya ulinzi huku akisisitiza kuzidi kuimarishwa katika michezo ijayo.
Hii leo
Chelsea wanakazi maneneo ya London ya kaskazini watakapo kuwa wakiwakaribisha Shakhtar
Donetsk Stamford Bridge.
Ripoti ya mwamuzi yawaokoa Mancini na Balloteli.
Meneja Roberto
Mancini wa Manchester City huenda akapona adhabu ya shirikisho la soka barani
Ulaya UEFA kufuatia kumfokea mwamuzi Mdanish Peter Rasmussen katika mchezo
baina ya Manchester City na Ajax mchezo uliopiga usiku wa jana, baada ya ripoti
ya mchezo kutokumtaja.
Bosi huyo wa
City alionekana kushikwa na hasira baada ya filimbi ya mwisho kufuatiwa kunyimwa penati
katika dakika za mwisho mwisho za mchezo huo dhidi ya mabingwa wa soka nchini
Uholanzi Ajax.
Mapema katika
mchezo huo bao la Sergio Aguero lilikataliwa na mwamuzi baada ya mwamuzi huyo
kupiga filimbi iliyo ashiria Aleksandar Kolarov aliyepiga krosi alikuwa ameotea.
Katika hatua
nyingine, UEFA imethibitisha kuwa kocha huyo mtaliano huenda asikumbane na
adhabu yoyote kwani katika taarifa ya mwamuzi wa akiba hakuna maelezo yoyote
yanayo husiana vitendo vya kocha huyo wakati wa mchezo hata baada ya mchezo.
Mario
Balotelli naye amenusurika na adhabu hiyo kutokana na dakika za mwisho kutaka
kumvaa mwamuzi baada ya kuvutwa na mlinzi wa Ajax katika eneo la hatari lakini
kitendo cha kuzuiwa na nahodha wake Vincent Kompany kimepelekea taarifa
kutoandika juu ya tukio hilo.
Maamuzi haya
yanaweza kushangaza sana kwani ni hivi karibuni UEFA ilimpiga faini meneja wa Arsenal
Arsene Wenger na kumsimamisha kwa mchezo mmoja kufuatia maoni yake dhidi ya
mwamuzi aliyechezesha mchezo kati ya Arsenal na Barcelona mchezo ambao Arsenal
walifungwa mabao 3-1 mwaka 2011.
Wenger pia
aliadhibiwa baada ya kukabiliana na mwamuzi Damir Skomina baada ya mchezo wa
ligi ya mabingwa ambapo Arsenal walichapwa na AC Milan mchezo uliofanyika Emirates
Stadium.
Arsenal iko tayari kuanza mwezi mgumu
anasema Walcott
Winga wa Arsenal
Theo Walcott ameelezea imani yake kuwa washika mitutu wako tayari kukabiliana
na changamoto ya michezo ya mwezi huu.
Vijana hao
kutoka Kaskazini mwa London watakuwa na
vibarua pevu katika kipindi cha mwezi huu ambapo wataanza kucheza dhidi ya Fulham
na baadaye kukabiliana dhidi ya Tottenham kisha Montpellier michezo ambayo
itapigwa katika dimba la Emirates kabla ya kusafiri kuwafuata Aston Villa na Everton.
Amenukuliwa winga
huyo akisema,
“sasa tunaingia katika mwezi mgumu kwetu, hiki
ni kipimo chetu si tu kipimo cha fiziki lakini pia akili lakini nafikiri tuko
tayari kwa lolote”
Mbali na
hilo ameonyesha kufurahia sare ya jana dhidi ya Schalke, licha ya kwamba walianza
kwa kuwa mbele kwa magoli mawili.
Ferguson: Real Madrid, Barcelona
& Dortmund ndiyo wapinzani wa Man Utd.
Meneja wa Manchester
united Sir Alex Ferguson ameweka wazi kuwa timu pinzani na United katika
michuano ya ligi ya vilabu bingwa Ulaya ni Real Madrid, Barcelona na Borussia
Dortmund.
United inaongoza
katika kundi H na kama watataka kutinga katika hatua ya mtoano ya 16 bora basi
watalazimika kuifunga Braga usiku wa leo mchezo ambao unafanyika nchini Italia.
Ferguson anadhani
kuwa vigogo viwili vya Hispania na klabu nchini Ujerumani watakuwa hatari sana kuanzia
katika hatua ya mtoano.
Manchester
United imekuwa ikifunga goli katika kila mchezo msimu huu achilia mbali mchezo
wa ufunguzi wa msimu wa ligi nchini England ambapo walifungwa na Everton kwa
bao 1-0.
Katika michezo
10 ya mashindano mbalimbali kikosi cha Sir Alex Ferguson mkimefunga jumla ya
mabao 27.
No comments:
Post a Comment