Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Mario Gotze anadhani Lionel Messi anastahili kushinda tuzo
ya FIFA ya Ballon d'Or kutokana na uwezo wake katika kipindi cha mwaka mzima wa
2012.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Argentina ameshinda mara mbili tuzo hiyo yenye heshima
kubwa duniani lakini mara zote amekuwa akikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka
kwa mreno Cristiano Ronaldo mbali na wachezaji wengine katika kipindi hiki.
Kama hiyo
haitoshi , Gotze amesisitiza kuwa nyota huyo wa Barcelona anastahili kushinda
kwa mara ya tatu na kusema waziwazi kuwa atampigia kura mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 25 kama atapewa nafasi ya kufanya hivyo.
Amenukuliwa akisema,
"nadhani
Messi atashinda Ballon d'Or kwa mara nyingine tena. Nitampigia kura".
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ujerumani pia amegusia mchezo wao ujao wa ligi ya mabingwa
ulaya katika kundi D mechi ya ugenini dhidi ya Real Madrid.
Amesema,
"kucheza
Santiago Bernabeu ni kitu muhimu bila shaka naelekea huko kwa furaha kubwa".
"Madrid
ni timu nzuri, kila mchezaji anaheshimika ninamatumaini mchezo utachezwa na
kumalizika Bernabeu halafu tutaelekea Dortmund kurudiana.
"naona
tutafuzu katika hatua hii ya makundi"
Alonso:
Steven Gerrard anatosha kuchezea Hispania
Kiungo wa Real
Madrid Xabi Alonso amempongeza nahodha wa Liverpool Steven Gerrard, akisema
kama angezaliwa nchini Hispania basi angeichezea timu ya taifa
ya nchi hiyo.
Kiungo huyo
wa wekundu wa England jumapili alikamilisha mchezo wa 600 kwa timu yake yenye
maskani yake pande za Merseyside na kukisaidia kikosi cha meneja Brendan
Rodgers kwenda sare ya kufungana bao 1-1 na Newcastle mchezo uliofanyika Anfield.
Alonso ambaye
aliwahi kucheza na kiungo huyo mzaliwa wa kitongoji cha Huyton kwa miaka mitano
kati ya 2004 na 2009, anaamini kuwa Gerrard ana ubora unaofanana na akina Andres
Iniesta, Xavi nay eye mwenyewe.
Amenukuliwa kupitia
television ya klabu yake ya Real Madrid akisema,
"haina
wasiwasi anaweza kuchezea timu yoyote ya taifa duniani kwasababu ana vitu vingi
vya ubora wa mchezaji"
Mancini anasema mchezo dhidi ya Ajax
ndio nafasi ya mwisho kwa Manchester City.
Bosi wa Manchester
City Roberto Mancini ameeleza kuwa mchezo dhidi ya Ajax hii leo wa michuano ya
ligi ya mabingwa ni nafasi ya mwisho kwa City kuendelea katika michuanoi hiyo
ya vilabu barani ulaya.
Mabingwa hao
wa soka nchini English tayari walikwisha kuadabishwa na vijana wa kocha Frank
de Boer msimu huu lakini pia wakichapwa na Real Madrid na wakaenda sare dhidi
ya Borussia Dortmund na sasa wakichungulia njia ya kutokea.
Lakini licha
ya Joleon Lescott na James Milner kuungana na David Silva, Jack Rodwell na Maicon katika orodha ya wachezaji majeruhi,
Mancini anasisitiza kuwa wale wazima katika kikosi chake watafanya kazi ya
kukabiliana na wapinzani wao usiku huu.
Anasema,
"tunawachezaji
muhimu kadhaa ni majeruhi lakini kama una tatizo wengine inabidi wafanye juhudi
uwanjani”
"hii ni
nafasi ya mwisho kwetu"
Ameendelea kusema
kikosi chake hakikuwa katika hali ya kimashindano ya ulaya huku akisema sababu
kubwa ni kwamba huu ni mwaka wa pili klabu yake kuwa katika michuano mikubwa kama hiyo.
No comments:
Post a Comment