KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 6, 2012

SIMBA SPORTS CLUB: HAKUNA ALIYEJIUZULU SIMBA SI KABURU WALA RAGE. KASEJA HASTAHILI LAWAMA NA MWANACHAMA MKOROFI TUTAMSHUGHULIA.

Klabu ya simba imekanusha taarifa za viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu kutokana na kuwepo taarifa zilizo nukuliwa hii leo katika baadhi ya vyombo vya habari juu ya kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi wa klabu hiyo. 

Akiongea na waandishi wa habari hii leo afisa habari wa klkabu Ezekiel Kamwaga hizo ni za uzushi zenye lengo la kupotosha na kuingiza klabu hiyo katika mtafaruku ambao haupo. 

Kamwaga amesema hakuna kiongozi yoyote aliyejiuzulu wala mjumbe wa kamati ya utendaji na kwamba taarifa hizo zimewasikitisha viongozi waliotajwa ambao ni mwenyekiti Ismail Aden Rage na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu.

 Amesema uongozi wa klabu hiyo umefanya kazi kubwa na unaendelea kufanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya usajili kwa kutumia pesa ya klabu jambo ambalo linadhihirisha uwezo mkubwa wa viongozi hao wanaojituma katika kuitumikia klabu hiyo. 

Amewataka wanachama na wapenzi wea klabu hiyo kuwa watulivu na kukubali matokeo ya kimchezo katika ligi kuu ya soka Tanzania bara ambapo Simba katika michezo ya hivi karibuni imekuwa ikifanya vibaya na kwamba hayo ni matokeo ya kimchezo ambayo yanaweza kutokea katika timu yoyote.

 Kamwaga amesema ligi bado ni ndefu kwani kuna mzunguzo wa pili unakuja ambapo viongozi na benchi la ufundi wanayafanyia kazi matatizo yaliyojitokeza katika michezo ya hivi karibuni ili kurejea katika mwenendo mzuri wa kimatokeo.

 Katika hatua nyingine msemaji huyo ametoa tahadhari kwa wanachama ambao wana nia ya kuanzisha vurugu ndani ya klabu hiyo kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu kama wataendelea na vurugu ambazo hazina msingi ndani ya klabu. 

Wakati hayo yakiwa hivyo Kamwaga amemtetea mlinda mlango wa Simba Juma Kaseja ambaye amekuwa akilaumiwa kuihujumu timu ya Simba hasa baada ya matokeo ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo ambao Simba walifungwa kwa mabao 2-0 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. 

Kamwaga amesema Kaseja ni miongoni mwa wachezaji waadilifu ndani ya Simba na pia ni mwenye kujituma na uchungu mkubwa na timu hivyo basi kumtuhumu kwa hujuma za kimakusudi ni kumuonea mlinda mlango huyo.

 Amesema kuwa jambo lililofanywa na baadhi ya wapenzi wa Simba wakati timu ikirejea kutoka mkoani Morogoro ikiwa njiani baadhi ya wapenzi wa Simba walitaka kumshusha Kaseja kwa lengo la kumfanyia kitu kibaya haikuwa sahihi na kwamba kitendo hicho kilikuwa ni cha kihuni ambapo pia waliomtolea maneno machafu ambayo hayavumiliki. 

Amewataka wapenzi wa Simba kuwa waaungwana na kuachana na vitendo vya aina hiyo hasa kwa mchezaji mwenye historia nzuri ndani ya klabu na taifa kwa ujumla.

 Jana Rockersports ilishuhudia baadhi ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wakiwa wameshika mabango yaliyokuwa na ujumbe unaotaka makamu mwenyekiti Kaburu na mlinda mlango Juma Kaseja kuondoka ndani ya klabu hiyo na kuwaachia klabu yao. 

Mabango hayo yalikuwa yakionyeshwa hovyo  hovyo karibu na viunga vya makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment