Shirikisho la soka nchini TFF limefanya marekebisho ya ratiba ya michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara kutokana na kuwepo kwea mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao utachezwa katika tarehe ya kalenda ya shirikisho la soka duniani fifa (fifa date)
Marekebisho hayo yametangzwa leo na katibu mkuu wa shirikisho hilo Angetile Osea katika makao makuu ya shirikisho hilo.
Osea amesema Taifa Stars itakuwa na mchezo tarehe 14/11/2012 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam licha ya kwamba bado haijathitishwa itacheza na nchi gani lakini ni vema marekebisho ya ratiba yakafanyika wakati huu wanaendelea na mchakato wa kuthibitisha timu ambao itakuja nchini kucheza mchezo huo.
Michezo ambayo itaathirika na mabadiliko hayo ya ratiba ni pamoja na mchezo baina ya Simba na Toto Afrika, JKT Oljoro dhidi ya Ruvu Shooting pamoja na mchezo baina ya Tanzania Prisons dhidi ya JKT Ruvu michezo ambayo hapo kabla ilikuwa ichezwe tarehe 11/11/2012 na sasa imerejeshwa nyuma kwa siku moja.
Mchezo wa Yanga na Coast Union uliopangwa kuchezwa tarehe 11/11/2012 wenyewe utaendelea kuchezwa katika siku hiyo kama ilivyokuwa umepangwa toka awali.
Osea amesema sababu kubwa ni kwamba kocha mkuu Kim Poulsen ambaye anatarajia kutaja kikosi hapo kesho ameomba kupata siku mbili za matayarisho ya mchezo huo na kwamba wao kama TFF wamewasiliana na kamati ya ligi kuijulisha juu ya hilo nayo kimsingi imekubali kufanyike mabadiliko ya ratiba ili kutoa fursa kwa mtaalamu huyo kuandaa kikosi chake.
Amesema kuna umuhimu wa kucheza mchezo wa tarehe ya FIFA kuliko kutokucheza na kwamba usipocheza mchezo katika tarehe hiyo athari yake ni kupoteza alama za viwango vya ubora hivyo ni muhimu Tanzania ikacheza mchezo huo.
Bofya kusikiliza
No comments:
Post a Comment