KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 29, 2012

NADIRI HAROUB KANAVARO AMSHINDA HARUNA NIYONZIMA. ZANZIBAR HEROES SAFI SANA


 Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Khamis Mcha Khamis yalitosha kuipa ushindi timu ya taifa ya Zanzibar dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda( Amavubi) katika mchezo wa kundi C uliopigwa uwanja wa  Namboole jioni ya leo.

Mshambuliaji huyo alitumia makosa ya mlinda mlango wa Rwanda Jean Claude Ndori kushindwa kuondosha mpira wa pasi ya kurejeshwa kwa mlinda mlango huyo kunako dakika ya 8 ya mchezo. 

Tangu wakati huo  Zanzibari ilitawala mchezo na pengine ingeongeza bao lingine katika kipindi cha kwanza lakini umaliziaji mbaya pengine kutokana na uwanja kuwa na matope.

Katika kipindi cha pili Amavubi ilirudi na ari nyingine kwa lengo la kusawazisha bao kupitia kwa Jean Baptiste Mugiraneza na Haruna Niyonzimana lakini mlinda mlango wa Zanzibar Mwadini Ally alikuwa imara kuzuia mipira ya hatari.

Zanzibar iliandika bao la pili kupitia tena kwa Khamis Mcha Khamis baada ya kupokea mpira wa shambulizi la kushtukiza kunako dakika ya 62 akipokea pasi ya nzuri kutoka kwa Kassim Suleyman toka upande wa kulia wa uwanja. 

Rwanda haikukata tama na juhudi zao zilizaa matunda zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kumalizika kwa bao Dady Boril aliyetokea benchi.

Mchezo huo uliwakutanisha manahodha wawili wa timu hizo za taifa ambao wote wanachezea timu moja ya Yanga ambao kabla ya mchezo kuanza walisalimiana kabla ya kubadilishana bendera za mataifa yao.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la C Malawi iliichapa Eritrea mabao 3-2 na hivyo kufanya kundi hilo kuwa katika mlingano unaofanana kwa maana ya timu ina nafasi ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali. 

Zanzibar inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 4 ambapo Rwanda na Malawi zikifuatia huku kila moja ikiwa na alama 3 na Eritrea ikiwa na alama 1.

No comments:

Post a Comment