Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeidhinisha jumla ya
wachezaji saba waliochaguliwa na makocha wa timu ya taifa katika mashindano
maalum yaliyofanyika tarehe 6/11/2012 mwenge Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu wa chama cha ngumi za ridhaa nchini Makore
Mashaga imewataja wachezaji waliochaguliwa na kuidhinishwa kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa dhidi Zambiakuwa ni pamoja na,
1. Said Hofu 49 Kgs Light Fly
2. Amdani Issa 52 Kgs Fly Weight
3. Frank Nicolas 56 Kgs Bantam
4. Ismail Galiatano 60 Kgs Light Weight
5. Kassim Hussein 64 Kgs Light Welter
6. Mohamed Chibumbui 69 Kgs
Welter Weight
7. Gulushid Rashid 75 Kgs Middle.
Jumla
ya wachezaji 15 wanaendelea na mazoezi uwanja wa ndani wa taifa chini ya
makocha Juma Selemani, Said Omari na Mussa Maisori.
Mashindano
ya kimataifa ya Tanzania na Zambia
yatafanyika katika ukumbi wa DDC Kariakoo tarehe 10/11/2012 kuanzia saa 9.00
Alasiri.
Mgeni
rasimi anatazamiwa kuwa Mh. Iddi Azzan (MB) Kinondoni.
Lengo
la mashindano hayo ni kuipatia timu yetu taifa uzoefu wa kaimataifa kabla ya kushiriki
mashindanao makubwa ya kimataifa kama ya
Jumuiya ya Madola ,mashindano ya Afrika na Olimpiki.
Wito
kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yetu ya Tanzania
kwa kuchangia kiingilio cha Tsh 10,000/= kwa Tsh 5,000/=.
Aidha
taarifa kutoka shirikisho la ngumi la Zambia
iliyotumwa na Rais wa shirikisho la ngumi Zambia
ndugu Thomas Chileshe zimeeleza kuwa wachezaji wa zambia wameondoka leo kwa njia ya
barabara na kesho wanatarajia kufika Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment