Ukiwa umesalia
mchezo mmoja kabla ya duru la kwanza la ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu ya
2012/2013 kumalizika, klabu ya Azam fc inayoshiriki ligi hiyo imesema bado
wanaimani kubwa kuwa msimu huu wa ligi ni msimu wao wa mafanikio zaidi na
watamaliza ligi hiyo wakiwa machampioni.
Azam mpaka sasa katika michezo yake ya ligi imeshinda
michezo 7, kwenda sare michezo 3 na kupoteza michezo 2 imefanikiwa kukusanya
alama 24 ikiwa katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
Akiongea na
Rockersports mara baada ya mchezo wake dhidi ya JKT Oljoro mchezo uliopigwa
katika dimba la Azam Complex na Azam kushinda kwa bao 1-0, kocha mkuu wa timu hiyo Stuwart John Hall amesema
anaamini hayo ni matokeo mazuri mpaka kufikia hapo.
"unajua tunataka kushinda kila mchezo na vijana wangu wanajua hivyo kwahiyo kupata goli moja si kitu kibaya sana japo lengo ni kushinda magoli zaidi'
"katika uwanja wa nyumbani vema ukashinda,
Oljoro ni wazuri ndio maana mchezo ulikuwa mgumu lakini kizuri ni kuwa hatujapoteza"
Amesema kuwa lengo kuu la klabu yake ni kutwaa
ubingwa wa ligi msimu huu na kwamba matokeo ya jana yamewaweka katika nafasi ya pili nafasi ambayo anaamini si mbaya na kwamba dhamira ya Azam na mara kadhaa
amekuwa akiwakumbusha vijana wake juu ya hilo ni kutwaa taji msimu huu.
Baada ya
kumalizika kwa mchezo wao wa jana dhidi ya JKT Oljoro Stewart Hall alisema
matokeo hayo yalikuwa muhimu kwa timu
yake na kusikitishwa na nafasi za wazi alizokosa Bocco lakini ameridhishwa na
kiwango chake na ushindi huo.
Stewart
amesema muda huu mchache ulibakia ataendelea kukifua kikosi hicho ili kumalizia
mechi ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT siku ya Jumamosi.
Tangu kurejea nchini kwa kocha huyo aliyeifundisha kwa muda mfupi Sofapaka ya nchini Kenya, Azam imecheza michezo mitatu ambapo ameshinda michezo miwili dhidi ya Coast Union bao 4-1 na jana dhidi ya Oljoro bao 1-0 lakini ilipoteza dhidi ya Yanga kwa kufungwa bao 2-0.
Azam FC
itaelekea mkoani Tanga, tayari kumalizia mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa
kwanza wa ligi kuu dhidi ya Mgambo JKT, utakaochezwa Jumamosi Nov 10 kwenye
Uwanja wa Mkwakwani mkoani humo.
No comments:
Post a Comment