Kocha wa Manchester City Roberto Mancini. |
Kocha wa Manchester City,
Roberto Mancini, amesema klabu hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa kufuatia
kushindwa kwa bao moja kwa bila na Sunderland.
Mabingwa hao watetezi, walipoteza nafasi nyingi
za kufunga wakati wa mechi hiyo, na kupoteza alama tatu muhimu, hatua
inayowaweka alama saba nyumba ya vinara wa sasa Manchester United.
Man City imefunga magoli 34 baada ya kucheza
mechi 19, katika mechi za ligi kuu msimu huu, idadi ambayo ni magoli
kumi na nne chini ya magoli waliyofunga mahasimu wao Manchester United
ambao waliilaza Newcastle 4-3 siku ya Jumatano.
Zaidi ya yote Man City imefunga magoli 12 kwa
mechi tisa za ugenini ukilinganisha na United ambayo imefunga magoli 22
kutoka kwa mechi 10.
No comments:
Post a Comment