Kikosi cha wachezaji
27 na viongozi 7 wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga kinatarajiwa
kuondoka jijini Dar es Salaam hapo kesho kutwa alfajiri ( jumapili) kuelekea Antaria nchini Uturuki kwa
ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili, ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa
ligi kuu ya soka Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari.
Akiongea hii
leo na waandishi wa habari, katibu mkuu wa klabu hiyo Laurence Mwalusako
amesema tayari matayarisho ya safari hiyo yamekamilika na kwamba msafara huo
utaongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji Mohamed Nyenge.
Amesema timu hiyo
itaondoka nchini saa 10:00 alfajiri ya Jumapili na inatarajiwa kuwasili katika
jiji la Instabul saa 4:50 asubuhi kabla ya kuelekea katika mji wa Antaria ulioko
kusini mwa nchi ya Uturuki ambako timu nzima itawasili huko majira ya saa 9:00
alasiri.
Yanga
itafikia katika Hoteli Sueno beach Hotel iliyoko katika mji wa kusini mwa
Uturuki wa Antari ambako ndiko hasa itakuwa ikiweka kambi yake katika kipindi
chote cha ziara yao ya kimazoezi nchi humo.
Mwalusako
amesema wachezaji wa Yanga wataelekea uwanja wa ndege wa mwalimu Julias Nyerere
saa 6 usiku wa kesho na kwamba kwakuwa msafara una watu wengi hivyo wameonelea
kufika uwanjani hapo mapema ili kukamisha taratibu za ukaguzi na mambo mengine
mapema.
Kwa upande
wake afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto amewataja wachezaji wataondoka
kuwa ni magoli kipa watatu Alli Mustafa, Saidi Mohamed na mlinda mlango
aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili Yusufu abdul.
Walinzi ni Shadrack
Nsajigwa,Oscar Joshua, Godfrey Taifa, Juma Abdul, Stephano Mwesika, Nadir
Haroub Kanavaro, Kelvin Yondani, Ladislaus Mbogo, na John Twite Mbuyu.
Viungo ni Nurdin Bakari,
Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani, Frank Domayo,
Athimani Iddi Chuji, David Luhende.
Washambuliaji ni Kabange Twitte,
Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Rehani Kibingu,Simon Msuva, Hamisi kiiza na George
Banda.
Benchi la ufundi
litaongozwa na kocha mkuu Ernest Brandts na msaidizi wake Fred Felix Minziro
pamoja na kocha wa makipa Razaki Omari Siwa.
Pia Yanga
itaondoka na daktari wa timu Sufiani Juma, meneja Hafidhi Salum na afisa habari
Baraka kizuguto.
BOFYA KUMSIKILIZA KIZUGUTO
No comments:
Post a Comment