KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, December 25, 2012

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA: DOWNINGI WA LIVERPOOL SASA SAFI. Liverpool kumuongeza mkataba nahodha wao Steven Gerrard na Barcelona wawataka Asernal kuachana na David Villa hauzwi januari.

Stewart Downing.
 Winga huyo alikuwa akihangaika katika kipindi kirefu tangu ajiunge na klabu hiyo majira ya kiangazi mwaka 2011 kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 20 jambo ambalo lilipelekea Liverpool kutaka kumuuza mwezi Januari lakini sasa mwingireza huyo amefanikiwa kuimarisha kiwango chake na sasa atasalia Anfield.

Amekaririwa meneja Liverpool Brendan Rogers akisema
"ndani ya kipindi cha wiki sita mpaka saba uwezo wake umeimarika na amekuwa akicheza katika nafasi mbalimbali, nilifurahishwa naye alipokuwa dimbani katika mchezo dhidi ya Fulham jumamosi. 

Alifunga goli , alitengeneza goli na alikuwa sawasawa. Alicheza pia vizuri dhidi ya Aston Villa katika eneo la ulinzi wa pembeni.
Uchezaji wa Downing umemvutia Rodgers kiasi kuelezea kuwa anataka mchezaji huyo asalie Anfield kwa kipindi kirefu zaidi.


Te Klose ameazimwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa  Chivas de Guadalajara.
Kikosi cha Chivas.
 Dennis Te Klose anakuwa Rais mpya wa shughuli za uendeshaji michezo katika klabu ya Chivas na Chivas USA,klabu ya Guadalajara imetangaza hapo jana.
Mduchi huyo ana uzoefu wa miaka 10 katika masuala ya soka nchini Mexico, ambapo pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa michezo wa Chivas USA katika kipindi kifupi wakati huo klabu hiyo ikianza shughuli zake za uendeshaji wa klabu. Alianza kazi katika soka kama mtafuta wachezaji wa Chivas.

Te Klose kwa kipindi kirefu pia amefanya kazi kama mkurugenzi wa soka la vijana katika shirikisho la soka la nchini Mexico. Alisifika kama mtu mwenye uwezo wakuona vizuri na kutambua vipaji katika shirikisho la soka la Mexico na vilabu vya vijana huko Tigres.


Steven Gerrard kuongezwa mkataba Liverpool.
 Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anataka kumuongezea mkataba kiungo Steven Gerrard akisema kiungo huyo bado ana mengi yakutoa katika uchezaji wake.

Mkataba wa sasa wa Gerrard Anfield unatarajiwa kumalizika kuelekea kumalizika kwa msimu wa 2013/2014.
Kiungo huyo wa kimataifa wa England amefunga jumla ya mabao 153 katika michezo aliyoitumukia Liverpool.

Amenukuliwa kupitia mtandao wa klabu Rodger akisema
"si dhani kama kuna swali lolote, tunataka kumuongezea mkataba".

Gerrard alianza kuitumikia Liverpool mwaka 1998 na kuiongoza klabu hiyo kama nahodha katika kipindi cha mafanikio cha kuchukua taji la ubingwa wa vilabu Ulaya mwaka 2004-05.
Akiwa na Liverpool ametwa mataji mawili ya FA na, League Cup mata tatu pamoja na taji la Uefa Cup.


 Zubizarreta: Barca haita muuza David Villa.
 Mkurugenzi wa soka wa Barcelona Andoni Zubizarreta amesisitiza kuwa amesema Arsenal iachane na wazo la kumununua David Villa mwezi Januari kwani mchezaji huyo hawatamuuza kwa kuwa klabu hiyo haina utaratibu wa kuwauza wachezaji wake muhimu katika kipindi cha nusu msimu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa katika vita kubwa ya kusaka nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hasa mara baada ya kufanikiwa kuponya maumivu ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua ambapo sasa inaarifiwa huenda akaondoka Barca mwezi January.
Arsenal imekuwa ikitajwa kuwa ikimtaka Villa lakini Barca wanasema hakuna mpango wowote wa uhamisho utakao fanyika mwezi January.

Amenukuliwa Zubizarreta na Canal Plus akisema
"mwezi januari tutaendelea kusalia na Villa na ni muhimu kukumbuka kuwa ni klabu ina tabia ya kukataa ofa za za mwezi huo, David ni mchezaji ambaye analeta magoli na uzuri wa kikosi
"sasa amerejea kutoka katika maumivu makali naamini kuwa anaendelea kuwa katika kiwango bora uwanjani licha ya kwamba ni kawaida kwa mchezaji mkubwa yoyte huwa anasaka nafasi ya kucheza na hilo ni zuri kwa ushindani wa kweli ndani ya kikosi"

No comments:

Post a Comment