KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 6, 2013

BAADA YA KUWAHENYESHA WAJERUMANI YANGA KURUDI GYM KUKAZA MSULI.

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football.
Kikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ambao uliishia kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Adora football Belek - Antalya.
Kocha Brandts ameendelea kukifua kikosi chake na kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo.
Arminia Bielefeld ambao awali hawakutegemea Tanzania kuwa kunaweza kuwa na timu ambayo inaweza kuwapa upinzani, walikiri mwishoni mwa mchezo kwamba Yanga ina timu nzuri na hawakutegemea kuona kiwango kizuri cha mchezo kilichoonyeshwa na vijana na wa Jangwani alisema mmoja wa maofisa wa Arminia Bielefeld.
Ukizingatia Armini Bielefeld ilikuwa imetoka kuifunga Bayern Levekursen 4-2 katika mchezo wa kombe la Ujerumani, walikutana na vijana wa Jangwani ambao waliweza kuutawala mchezo huo kuanzia kwa mlinda mlango Ally Mustafa 'barthez, mpaka kwa washambuliaji wake.
Brandts alisema amefarijika na matokeo ya mchezo huo, japokuwa lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata ushindi katika mchezo huo lakini wachezaji wake waliweza kufanya kazi nzuri sana uwanjani kitu kilichofanya Wajerumani kushangaa. 

Wachezaji wa Yanga leo jioni watakua wakifanya mazoezi ya kujenga mwili misuli (GYM) katika  Hotel ya Fame Residence Lara & Spa ambao kesho asubuhi itaendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence Football

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football.

No comments:

Post a Comment