Vincenzo
Montella ameelezea furaha yake baada ya kufanikisha usajili wa mshambuliaji mzaliwa
wa New Jersey, Giuseppe Rossi akitokea Villarreal wakati huu ambapo dhamira ni
kuhakikisha katika mwaka huu wa 2013 Fiorentina wanaanza na ushindi nyumbani
dhidi ya Pescara.
Kwasasa wenyeji
hao wa mji wa Viola wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya nchini
Italia Serie A, alama tisa nyuma ya vinara Juventus, na kocha anaamini kuwa
usajili huo ambao kwao unatazamwa kama usajili mkubwa ambao utawawezesha
kuelekea katika mwelekeo mzuri.
Rossi amekuwa
nje ya uwanja tangu mwezi Oktoba mwaka 2011 kutokana na kuumia mfupa wa mguu
anatarajiwa kurejea dimbani mwezi March.
Marseille iko tayari kumuuza Remy.
Mkurugenzi wa
michezo wa Olympique de Marseille, Jose Anigo amesema klabu yake iko tayari
kumuuza Loic Remy katika kipindi hiki cha majira ya baridi endapo bei ya
thamani ya mchezaji huyo itafikiwa.
Mchezaji huyo
wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na kuihama Marseille,
na lengo lake likiwa ni kutaka kuelekea katika soka la England.
Newcastle inaaminika
kuwa ndio kinara wa mbio hizo za kupata saini ya mshambuliaji huyo.
Anigo, ambaye
ndiye kiongozi wa usajili katika klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini
Ufaransa ‘Ligue 1’ amesema Remy huenda akaondoka Stade Velodrome mwezi huu
endapo pesa yenye thamani ya mchezaji huyo itafikiwa.
Bosi wa Swansea Laudrup anasema Michu
hataondoka mwezi huu wa January
Meneja wa Swansea
City Michael Laudrup amedai kuwa mshambuliaji wake Michu hawezi kuondoka katika
dirisha hili la usajili la mwezi wa January.
Mhispania huyo
amekuwa katika kiwango cha juu katika safu ya usahmbuliaji ya klabu hiyo tangu
kujiunga nayo kwa uhamisho wa pauni milioni mbili akitokea Rayo Vallecano msimu
uliopita na msimu huu akiwa amesha pachika wavuni jumla ya mabao 13 katika
jumla ya michezo 22 msimu huu.
Timu mbili
za nchini Russian, Zenit St Petersburg na Anzhi Makhachkhala zimeripotiwa
kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, lakini bosi huyo wa
Swansea amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo ataendelea kusalia Liberty Stadium mwezi huu.
No comments:
Post a Comment