Sir Alex
Ferguson amelikubali goli la kusawazisha la Manchester United baada ya
kufanikiwa kulazimisha sare dhidi ya West Ham mchezo wa michuano ya FA.
Mabao mawili
ya kichwa ya James Collins yaliyotokana na mpira wa krosi wa Joe Cole ambaye
amerejea kwa washika nyundo akiwa amependeza katika rangi za jezi ya West Ham
baada ya kuihama klabu hiyo karibu miaka 10 iliyopita na kuelekea Chelsea, yalikuwa
kidogo yawape ushindi wa mabao 2-1.
Hata hivyo
pasi murua ya mkongwe Ryan Giggs kwenda kwa Robin van Persie ambaye alimalizia
kwa kufunga bao la kusawazisha liliiokoa United kutopoteza mchezo huo na kufanikiwa kupata sare ya
mabao 2-2 katika dimba la Upton Park.
Meneja wa
United Sir Alex Ferguson amevutiwa na bao zuri la Van Persie la kusawazisha
akiwa katika msimu wake wa kwanza na klabu hiyo, akisema goli hilo lilikuwa
safi na anatarajia mengi makubwa kutoka kwa mduchi huyo.
"yuko
katika umri wa kupevuka sasa. Ameleta upevu katika safu ya ushambuliaji''
Mourinho awatolea uvivu wachezaji
wake awapasha hakuna mwenye namba ya kudumu.
Meneja wa Real
Madrid Jose Mourinho amewatolea uvivu wachezaji wake na kuwaonya kuwa hakuna
mtu mwenye nafasi ya kudumu katika kikosi cha Real.
Mlinda mlango
wa Iker Casillas hakupangwa katika katika mchezo ambao Real Madrid ilipoteza
kwa kufungwa magoli 3-2 na Malaga mwezi uliopita, jambo ambalo lilihatarisha
kibarua cha kocha huyo.
Mabingwa hao
wa Hispania hii leo wanakibarua dhidi ya Real Sociedad mchezo wao wa kwanza kwa
mwaka huu wa 2013 na Mourinho akigomea kuweka wazi kama Casillas atakuwepo
katika kikosi cha kwanza hii leo.
Alipoulizwa kuwa
ni nani atakuwa golini katika mchezo wa leo Mourinho alijibu kwa dhihaka
"wachezaji
wanajua nani atakuwa golini, unaweza kucheza leo lakini usiwepo katika mchezo
wa jumatano wa Copa del Rey jumatano”
"kujiamini
ni tafsiri ya kucheza vizuri, lakini kinachotakiwa ni kuwa katika kiwango
cha ushindani na kuwa na uwiano sawa katika kila nafasi. Kuwa katika matumaini
ya nafasi ya kudumu wakati mwingine si jambo jema"
Vilanova arejea kibaruani
Kocha wa Barcelona
Tito Vilanova hii leo anarejea kuongoza
kikosi cha timu yake dhidi ya Espanyol mchezo ambao ni wa timu zinazo toka
katika eneo moja yaani ‘derby’.
Vilanova mwenye
umri wa miaka 44, hivi karibuni alisumbuliwa na kansa ambayo iligundulika
katika mwili wake mwaka 2011 ambapo kocha huyo raia wa Hiaspnaia alilazimika
kufanyiwa upasuaji wa tezi ambapo kuelekea mwisho wa mwezi Rais wa Barca Sandro
Rosell alisema kuwa kocha wake atarejea kazini katikati ya mwezi January.
Msaidizi wa
Tito , Jordi Roura, amethibitisha kuwa Vilanova atakuwa kazini Camp Nou jumapili.
No comments:
Post a Comment