KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 6, 2013

KOMBE LA MAPINDUZI: MTIBWA YACHECHEMEA COAST UNION MDOGO MDOGO NA AZAM YAONGEZA KASI.


Ally Mohamed‘Gaucho’ akipambana na wachezaji wa Coastal Union, Othman Tamim na Suleiman Kassim ‘Selembe’ katika mchezo wa leo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. (Picha kutoka Zanzinews blog)


 Michezo miwili ya michuano ya kombe la Mapindizi visiwani Zanzibar imeendelea tena, ambapo katika mchezo baina baina ya Mtibwa sugar na Coast Union ya Tanga mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1.
Mtibwa ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi kitiwa nyavuni na Ally Mohamed dakika ya 57 ya mchezo nao Coast wakisawzisha kupitia kwa Jerry Santo kunako dakika ya 20 ya mchezo huo.

 MCHEZO WA PILI

Katika mchezo wa pili mabingwa watetezi wa taji la mapinduzi Azam wamechomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ngumu ya Miembeni mchezo ambao umepigwa katika dimba la Amani.
Mabao ya Azam fc yamewekwa kimiani na Joackins Atudo kabla ya Miembeni kusawazisha bao hilo kupitia kwa Adeyoum Salehe na baadaye mshambuliaji Gaudience Mwaikimba wa Azam kuandika bao la pili kwa timu yake.
Azam ilifanikiwa kuandika bao lake la tatu katika kipindi cha pili likifungwa na
Uhuru Suleiman dakika za mwisho wa mchezo.
Azam sasa inashika usukani kwa alama 4 ikifuatiwa na Miembeni yenye alama 3, Coast alama 2 na Mtibwa alama 1.

No comments:

Post a Comment