Wakala: Lampard lazima aondoke Chelsea.
Imethibitika
kuwa Frank Lampard ataihama Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa
wakala wake Steve Kutner.
Akikaririwa na
magazeti ya nchini Uingereza akisema,
"watendaji
wa Chelsea walimwambia Frank kule Japan wakati wa michuano ya kombe la dunia la
vilabu na hata mara baada ya ushindi dhidi ya Everton mwezi uliopita kuwa
hakuna chochote kitakacho pelekea klabu kumpa ofa nyingine Lampard baada ya
msimu huu"
"hakuna
kitakacho badilika kwa vyovyote vile. Frank anapashwa kukubaliana na hayo
inabidi ajikusanye kumalizia msimu kwa mafanikio katika klabu ambayo aliipenda
sana."
Lampard alipata
nguvu mpya kutokana na kushangiliwa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa
mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Southampton jumamosi pale
alipofunga goli ambalo kimsingi lilimfanya kuwa sawa na mchezaji wa zamani klabu
hiyo Kerry Dixon mwenye rekodi ya juu ya ufungaji magoli, lakini inaonekana
sherehe ya ushangiliaji baada ya kufunga goli akiwa katika jezi yake maarufu namba
8 mgongoni inaelekea ukingoni.
Mashabiki wa
Chelsea wamekuwa wakitaka Lampard apewe mkataba mwingine lakini hali inavyo
onekana ni kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Stamford Bridge.
Mwenyewe Lampard
amekaririwa akisema
"pengine
sikuwa na mvuto wa kutosha lakini mashabiki wamekuwa na mimi katika kipindi
chote ambacho tumekuwa pamoja hapa"
Rodgers amtetea Suarez baada ya mpira
wa mkono.
Brendan
Rodgers: 'Nadhani haikuwa makusudi ya mwamuzi'
Brendan
Rodgers amesema goli la ushindi la Luis Suarez ambalo lilitokana na mpira uliotengenezwa
kwa mkono kabla ya kufunga kwa mguu wa kulia halipaswi kuendelea kuzungumziwa
aambapo pia amemsifia mshambuliaji huyo baada ya mchezo huo kati ya Liverpool
na Mansfield.
Luis Suarez aliutuliza
mpira kwa mkono kabla ya kufunga goli, ambalo lilikubaliwa na mwamuzi na kutoa
matokeo ya ushindi wa kwa Liverpool.
Liverpool inajipanga
na mchezo wa mzunguko wa nne wa michuano hiyo ya FA dhidi ya Oldham Athletic baada
ya kupata goli la fuluku na kupelekea ushindi wa mabao 2-1 katika dimba la One
Call Stadium.
Daniel
Sturridge alifunga goli lake la kwanza katika timu yake mpya ya Liverpool dakika
ya saba kabla ya Suarez kuandika bao la pili baada ya kuingizwa uwanjani kipindi
cha pili.
Kelele za
kuzomea zilisikika uwanja mzima baada ya goli hilo kuruhusiwa, ambapo licha ya
jitihada za wenyeji kuweka mpira kati na kuanza kwa lengo la kusawazisha jitihada
zao hazikuza matunda ili kupata mchezo wa marudiano kule Anfield.
Akikaririwa Rodgers
amesema,
"nimeona
hakuna shaka yoyote kuwa ulikuwa ni mpira wa mkono, nadhani walichokiona
waamuzi ni kuwa haikuwa makusudi, na ni wazi kabisa haikuwa makusudi.
"nilimuuliza
mwamuzi wa akiba baada ya mchezo kama ulikuwa ni mpira wa mkono kwa kuwa
sikuona moja kwa moja alinijibu ni kweli. Kwa hiyo ni wazi ilikuwa bahati mbaya
kwa Mansfield na bahati kwetu kupata goli."
No comments:
Post a Comment