Ernest Brandts akiwa mazoezini asubuhi ya leo kutoka kushoto ni Saidi Bahanuzi, Haruna Niyonzima na Simon Msuva. |
Ernest Brandts na Minziro wakiongoza mazoezi asubihi ya leo. |
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Denizlispor FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uturuki mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Selen
Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Yanga ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya kwa wiki mbili itatumia mchezo
huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo
imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapamabana
kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina
wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi
na kuwavutia.
Baada
ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya
Armini Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine
nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia
kuona maendeleo ya kikosi kutokana na mazoezi ambayo wamekuwa wakifanya tangu walipofika Antalya
Denizlispor FC ni
miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambazo
zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko
wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji
wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na
Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni
miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young
Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari
kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen
Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na
hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd
'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa
juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizuri na wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini
Antalya.
Kuhusu hali ya
hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana
kuimudu na muda mwingi kwa sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu
wakati wa mazoezi mpaka mida ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi
joto 17 - 21, hivyo hali ya hewa ni nzuri tu.
No comments:
Post a Comment