KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, January 12, 2013

BONANZA KUBWA LA WACHEZAJI WALIO TISHA KWENYE VILABU NA TIMU YA TAIFA KWA UDHAMINI WA NMB UWANJA SIGARA JUMAPILI HII NJOO UWAONE HAWA HAPA CHINI NA WENGINE KIBAO.

Kikosi cha Simba kutoka kushoto ni Barnabas Sekelo, Dua Bin Said, Bita John, Iddi Seleman 'Kibodya' Abdul Mashine na Yusufu Macho 'Musso' . Kutoka kushoto waliochuchumaa ni Waziri Salum, Spear Mbwembwe, Hussein Balo, Abubakar Kombo na Saidi Msasu.
Kikosi cha Reli ya Morogoro waliosimama kutoka kushoto ni Godfrey Kikumbizi, Yahya Issa, Athumani Msumari na wa mwisho ni Cristopher Alex. Waliochuchumaa kutoka kushoto wa 
kwanza nimemsahau wa pili ni Abeid Kasabalala, Peter Mjata, Mohamed na Wema Juma.
Waamuzi wa zamani Athumani Kazi, mzee Christopher Makwega na mzee Hamisi Kisiwa.
  Lile Bonanza kubwa linalo wajumuisha kwa pamoja wachezaji walikuwa wakali katika vilabu mbalimbali nchini Tanzania wakati huo kuanzia miaka ya 70 mpaka miaka ya 90 litaendelea tena jumapili hii katika uwanja wa Sigara Changombe jijini Dar es Salam.
Jumla ya timu 9 tayari zimethibtisha kushiriki ikiwemo Yanga ambayo katika Bonanza la mwezi wa Novemba iliingia mitini.

Kudhihirisha ya kwamba Bonanza lililopita lilikuwa zuri na kusisimua wadau wengi wa soka hapa nchini, safari hii benki ya NMB imejitokeza kudhamini bonanza hilo.

Akiongea na Rockersports mratibu wa bonanza hilo Kennedy Mwaisabula(maarufu kama mzazi) amesema ana imani kubwa Bonanza la mwezi huu wa Januari litakuwa zuri zaidi ya mwezi Novemba hususani kufuatia kupata udhamini wa NMB.

Kikosi cha Plisner kutoka kushoto waliosimama ni Jarufu Karenga, Kaingilila Maufi, Roman Paul, Eustus Bajwala na Shabani Ramadhani. Walioinama ni kutoka kushoto ni Issa Kayeyo, Abuu Rajabu, Francis Modest Mwanga na Mwavanga Kihwelo.
Amesema anaishukuru benki hiyo kwa kutambua mchango wa wachezaji wakongwe katika taifa hili na kukubali kuwapa sapoti na hivyo kuwataka na wadau wengine mashirika, taasisi binafsi, mashirika na makampuni mbalimbali kujitokeza kuchangia mabonanza ya kila mwezi na vilevile kwenda kuangalia wachezaji hao wa zamani.

"Tunaishukuru benki ya NMB kwa kutambua mchango wa wachezaji wa zamani kwa kukubali kudhamini bonanza hili, na wengine wafuate nyayo za NMB", alisema Mwaisabula.

Timu za zamani ambazo zinashiriki kwenye bonanza hilo ni zile zilizowahi kutamba hapa nchini katika ligi kuu ya Tanzania (wakati huo ikiitwa ligi daraja la kwanza) na kwamba Bonanza litaanza saa 2:00 na kwamba timu ambazo hazijakamisha taratibu zifanye hivyo kwa kuitumia siku ya leo kukamilisha ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya ushiriki.

Timu hizo ni Simba, Yanga, Ushirika, Tukuyu stars, Pamba ya mwanza, Bandari ya Mtwara, Reli ya Morogoro, Pilsner, Coastal union, Kariakoo Lindi. 

Tatari timu za Simba, Yanga na Bandari zimekamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na ada ya ushiriki wao.

Bonanza hili ni la pili kufanyika baada ya lile la kwanza lililofanyika Novemba 18 mwaka jana, ambapo Milambo ya Tabora ilifungwa magoli 3-2 na Bandari Mtwara, Reli Morogoro iliifunga Plisner ya Dar 1-0,Simba ilitoka sare na Kariakoo Lindi ya mabao 2-2 na Ushirika Moshi ilicheza na Kombaini baada ya kuwa na timu saba

No comments:

Post a Comment