Timu ya taifa ya Tanzania iliyokuwa dimbani la taifa la Addis jioni ya leo ikicheza dhidi ya timu ya Taifa ya Ethipia imepoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 2-1.
Akiongea na Raockersports afisa habari wa shirikisho la soka nchi Bonface Wambura aliyeambatana na timu hiyo amesema Ethiopia walianza kuandika bao la kwanza kunako dakika ya 15 lililofungwa na Fuad Ibrahim bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Stars walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji Mbwana Samata kunako dakika ya 51 kabla ya wenyeji kuandika bao la pili kupitia a Bekele kunako dakika ya 69.
Stars walikuwa wakiutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya mchezo wa makundi kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia 2014 dhidi ya Morocco na wao Ethiopia wanajiandaa na safari ya kuelekea nchini Afrika kusini kwenye fainali za mataifa ya Afrika AFCON ambao wataanza fainali hizo dhidi ya mabingwa wa Afrika Zambia ukiwa ni mchezo wa kundi C.
No comments:
Post a Comment