Liverpool itaingia katika mbio za kumnasa Wesley Sneijder endapo kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi atakubali kupunguza mahitaji yake makubwa ya mshahara anayotaka kwasasa.
ingawa Sneijder anaonekana hafanani na sifa za aina ya wachezaji ambao wamiliki wa Liverpool wa FSG wamekuwa wakiwalenga ambazo ni umri mkubwa wa miaka 28 na gharama ya mshahara wa pauni milioni 6 kwa mwaka lakini meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers ameonekana kumtamani kiungo huyo nguli.
Galatasary
ndio klabu pekee kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wa Inter Milan na sasa wanataka majibu ya mpango wa mchezaji huyo hii leo.
Sneijder anaonekana kuwa na wasiwasi juu ya kuelekea Uturuki na anadhani kuna haja ya kucheza soka karibu na nyumbani Uholanzi kutokana na sababu za kifamilia.
Inter
italazimika kuachia aondoke kwa pauni milioni £6.2 lakini kuelekea Anfield itategemea na punguzo la mshahara uliotakiwa na Sneijder mwenyewe.
Sneijder anafahamu kuwa masiha yake ya soka katika klabu ya Milan yanafikia mwisho mwezi huu lakini juu ya hatma yake ya baadaye amenukuliwa akisema.
Na hapa amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema
Na hapa amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema
'Tazama wachezaji wote ambao wako katika soko la uhamisho katika soko la wachezaji kipindi hiki wanaaamua nini cha kufanya kabla ya January 31, na mimi nitafanya hivyo o,'.
'sitaki kuharakisha na vilevile sitaki kuharakishwa.
'baada ya kila kitu kuwa kimekamilika sitaki kuwa katika fikra hizo za kulazimishwa kuchagua jambo la kimaisha.'
No comments:
Post a Comment