Manchester United imethibitisha kuwa Darren Fletcher atakosekana kwa sehemu yote ya msimu iliyosalia kutokana na kulazimika kufanyiwa upasuaji kuondoa tatizo sugu la tumbo ambalo limekuwa likimsumbua.
Fletcher mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akisumbuliwa kwa karibu miaka miwili na maumivu hayo kitaalamu yakitambuliaka kama 'ulcerative colitis' na United imesisistiza kuwa upasuaji huo ilikuwa ni sehemu ya mpango wao na kwamba hiyo itampa faraja hapo baadaye.
Kiungo huyo raia wa Scotland kwa mara ya mwisho kuonekana dimbani ilikuwa ni katika mchezo mchezo dhidi ya Newcastle United siku ya Boxing Day ambapo United ilishinda kwa mabao 4-3
ambapo aliingia akitokea benchi na kwa ujumla amecheza michezo 10 tu msimu huu baada ya kurejea mwezi kufuatia kuwa nje kwa miezi 10.
Taarifa ya klabu imesema,
‘Darren Fletcher atakosekana kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia kwani amefanyiwa upasuaji kuondoa tatizo lake la ulcerative colitis'.
Fletcher amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo tangu March 2011 ingawa kufuatia kukosekana kwa kipindi kirefu hapo awali kulikuwa kunatafsiwa pengine anasumbuliwa na matatizo yanayosababishwa na virus.
Baada ya kukosekana mwanzoni mwa kampeni ya kuanza msimu wa 2011-12, alirejea baadaye na kucheza michezo lakini baadaye tena akalazimika kupumzika kwa kipindi kirefu zaidi.
Si tu United itakayo athirika na hilo bali pia hata Scotland ambayo amekuwa akiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchini hiyo kama nahodha na sasa ikiwa chini ya Gordon
Strachan ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Estonia na baadaye michezo miwili ya kuwania kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Wales, Serbia na Croatia.
Hapa Fletcher akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya QPR mapema mwezi huu.
No comments:
Post a Comment