Rebrand: Uwanja Wembley Stadium uliopata udhamni wa EE unaonekana ukiwa katika matayarisho ya kubandikwa jina jipya baada ya mchakato wa kupata jina muafaka.
|
Chama cha soka nchini England FA kinafikiria kutoa jina jipya la uwanja mkubwa wa nchi hiyo wa Wembley Stadium kwa njia ya kuwashirikisha mashabiki wa soka wa nchi hiyo.
Katika mpango wa mkataba wa udhamini wa uwanja huo ilioripotiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 8 kutoka EE, uwanja huo wa kihistoria utakuwa ukijulikana kwa jina la kuunganisha jina halisi la uwanja huo la 'Wembley Stadium na kuhusisha kampuni ya watoa huduma za simu ya EE.
FA imekubali pia mpango kama huo katika michuano mikubwa ya soka nchini humo ya FA Cup, ambayo rasmi michuano hiyo itajulikana kama FA Cup kwa udhamini wa Budweiser.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia gazeti la Daily Telegraph,
ni kwamba FA imesisitiza kutaka juu ya umiliki wa haki ya jina kama ilivyokuwa kwa uwanja wa Arsenal ambao unaitwa uwanja wa Emirates na kwamba isije ikawa ni uporaji na kwamba neno 'Wembley' litasalia kama lilivyo.
Kwasasa Wembley umekuwa ukidhaminiwa na makampuni mengi ikiwa ni pamoja na Carlsberg ambao wamepewa haki ya kuwa bia rasmi ya uwanja wa Wembley.
Kampuni ya EE
iliundwa baada ya kuundwa kwa kampuni ya Orange and T-Mobile mwaka 2010. FA kwa muda mrefu imekuwa ikisaka mdhamini kiongozi wa uwanja tangu kufunguliwa kwake mwaka 2007.
Hapo zamani uwanja huo ulikuwa ukijulikana kama Empire Exhibition Stadium.
Swali - Unaonaje na sisi kwa uwanja wa taifa na uhuru tufanye kama hawa waliotutangulia katika mambo mengi ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na soka.
Ukitaka maendeleo jifunze kwa wenzako.
No comments:
Post a Comment