Timu
ya Yanga leo itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya
Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya
majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati
Yanga ambayo imeweka kambi ya mafunzo katika mji
wa Antalya imekuwa ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji
wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa
ujumla.
Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5)
mfiululizo itatumia mchezo wa leo jioni dhidi ya timu ya Arminia Bielefed
kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini
Uuturuki.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts
amesema anashukuru wachezaji wake wapo fiti kwa ajili ya mchezo
kesho, na kwa kuwa hakuna mchezaji majeruhi atakuwa na fursa ya kumtumi
amchezaji yoyote katika mechi hiyo.
Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo wa leo utakua
mgumu kwani timu ya Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekua ikishiriki
ligi kuu ya ujerumani mara kadhaa, hivyo ni timu ambayo itatoa
ushindani mkubwa sana
No comments:
Post a Comment